Monday, August 19, 2013

USIKU ULE WA KWANZA WA FUNGATE (HONEYMOON)......Part 5 (FINAL)!!!

Hello rafiki habari yako!
Naamini umekuwa unafuatilia sana habari hii
Iliyoanzia mbali saaana,pande hizi;
 
.......kwa pamoja wote wakamwambia Usijali,ahsante kama tutahitaji ushahidi wowote ule tutakutaarifu,basi meneja akatoka na kuwaacha na wao wakabaki na kuongea kitumishi na kiutu uzima na baada ya mazungumzo ya kina kiasi,basi wote kwa pamoja wakaamua ku……………………………….ENDELEA SASA!
 
 ....kutafuta suluisho kwa pamoja...Basi jambo la kwanza walilolifanya ni kukaa chini na kujadilina kwa kina nini cha kufanya,maana kama kijana akirejea nyumbani sasa peke yake itazua gumzo mtaani na kanisani,hivyo ni bora huyo kijana asafiri kidogo na kwenda kupumzika kwao mkoani angalau kwa siku kadhaa wakati ufumbuzi unatafutwa.
 
Basi walibembelezana hapo na wakawa imara, na hapo mama mkwe na mke wa yule msimamizi wakatoka nje na kuwaacha Yule mtumishi na msimamizi wake wa ndoa kwa muda fulani ili wazungumze kiume na kumsaidia kupanga nguo na zile zawadi kwa ajili ya kutoka hapo hotelini.
 
Naam yule msimamizi wa ndoa akataka kupata stori kwa ufupi,usiku ule ulikuwaje...Basi yule kijana akaanza kumsimulia kuwa tukiwa kwenye gari tunakuja huku hotelini toka ukumbini,Mke wangu alikuwa na hamu sana ya kushiriki tendo hili la kwanza hivyo alikuwa joto sana,na hata tulipoingia tu hotelini cha kwanza ilikuwa ni mashamu shamu kibao...lakini mimi niliazimia kuanza tendo hili la kwanza kwa kuweka wakfu kwanza kwa maombi....hivyo nilimshauri tufanye maombi,na hata tulipoanza yeye hakuomba wala hata kuwa na mimi sana,bali nikiwa ninaendelea yeye alitoka na kwenda kuoga na kurudi na Taulo tu,na kukaa mbele yangu hali ninaendelea kuomba na mimi nikaona hapa ipo shida,kwa hiyo nikazidi kutakasa na kukemea kila aina ya maroho machafu ndani ya mke wangu,baada kumaliza kuomba,kwa muda kama wa masaa mawili hivi nikaenda na mimi kuoga na niliporudi nikakuta mke wangu amepitiwa na usingizi,huku taulo imemfunuka na hivyo akiwa wazi kabisa.
 
Yule msimamizi akauliza ..yaani umefika honeymoon ndio unaanza kuomba? ulikuwa wapi siku zote? na huyo mke mpaka umepewa toka madhabahuni,yaani umekuja kugundua uchafu na maroho ukiwa nae huku hotelini? na hatukatai kuanza na maombi ukiwa honeymoon maana ni ibaada,lakini ndio wewe umeamua kufanya masaa mawili kweli? Jamani unajua kila jambo lazima lifanyike kwa utaratibu na kwa mpangilio tena kwa wakati wake!.....wakati yule bwanaharsi akijitahidi kujitetea, yule msimamizi akasema hapana utetezi katika hili mpaka hapo ulikuwa umeshamtesa sana kihisia na hivyo sio vizuri.
(Naamini na ninyi wasomaji mmepata fundisho katika hili,huwezi kuwa  kwenye uchumba ama mahusiano yeyote yenye kibali cha Mungu na usijue nini cha kuombea,eti mpaka wakati wa honeymoon...na hata kama wewe ni mtakatifu zaidi ya utakatifu wenyewe,lazima ujifunze kufanya kila jambo kwa wakati wake...ya kiroho yawe hivyo na ya kimwili yawe hivyo)
 
 Eeeh endelea kaka...
Basi nilivyotoka kuoga, nakumwona yuko vile nikaona sasa ndio wakati muafaka wa kuendelea na ibaada,basi nikamshtua taratibu,na kabla sijasema neno,aliponiona namuangalia basi basi akanirukia mwilini na kuanza mashamushamu tena,na kiukweli mimi mengine siyajui na yamkini sikuitikia vile anataka labda,basi akiwa anaendelea hapo tukaangukia kitandani nae akawa juu yangu na vurugu hizo,baada ya muda kidogo nikaona niko tayari,basi nikampindua na bila kuchelewa nikaingia...na hapo kuna namna ambayo alilamika...na kusema Mbona hivyo? na sikujua nini mbaya,basi tuliendelea na mimi nilipomaliza tu basi nikaona kwa leo kwasababu ya vurugu zote na mchana,na muda niliotumia kwenye maombi,basi nikajihisi kuchoka naam nikwambia yatosha kwa leo nami nikalala,nilimuona kama amekasirika kiasi ingawa alijifanya kufurahi na hapo alitoka na kwenda bafuni,nafikiri alienda kuoga mmmh!
 
Basi yule best akashangaa na kuumia mno na kusema umemtesa sana mke wako na hata kama sijui sababu hasa,yamkini na hiyo imechangia sana sana,na hapo akaanza kumpa shule kwa kina na hapa nitakuwa kwa ufupi shule yenyewe;
 ( Wanawake na wanaume wametofautiana sana kimaumbile,kihisia na kimuundo...wakati mwanaume akipata tu wazo au hamu ya kufanya mapenzi basi saa hiyo hiyo ama ndani ya muda mfupi sana huwa tayari lakini wanawake hisia zao hupanda taratibu sana hivyo anahitaji maandalizi ya kutosha,kwanza utayari kisaikolojia kisha juhudi za kuamsha hisia hizo....na wanaume wengi huwa hawajui kuwa wanawake nao hufika katika kilele cha furaha yao (ogarsm), na hivyo wengi hujifikiria wao tu,hivyo wanavyomaliza tu wao basi wanadhani ibaada imekwisha....kuna mamilioni ya wanawake duniani wanabakwa na waume zao kila siku,naam wengine wana miaka mingi kwenye ndoa zao na wana watoto lakini hawajawahi kufurahia tendo la ndoa hata kidogo....Mungu ametoa zawadi ya tendo la ndoa ili kwanza wanadamu walifurahie na matunda yake pia ni kupata watoto. Ndoa nyingi zina ugomvi sana hata wanandoa kutoka nje ya ndoa zao sio tu kwasababu shetani anawaendesha,hapana ila kutoridhishana ndio moja ya vyanzo vikubwa na ukiona unaanza honeymoon kwa majonzi basi huwezi kuifuta hiyo picha maishani mwako na mbaya zaidi ni pale dada ambaye alikuwa mfukunyuku huko duniani na hivyo anajua halafu mume hafiki pale juu,basi kumshika Mungu inakuwa hati hati....hivyo ni vema kumuandaa mkeo,angalau dakika 45 kabla ya tendo ili kujenga mazingira ya kibaiolojia ya utayari wake ili nae afanye bila kuumia na afurahie tendo hilo pia....ukiwa umeoa huna haraka ya kukimbia,maana huyo ni mkeo tu na ndio maana ya honeymoon...it is a sex orientation and affairs foundation....BASI IMEMPASA KILA MTUMISHI KULITAFAKARI JAMBO HILI)
 
Basi endelea kaka,naamini umenielewa(Alisema msimamizi)
Oooh kumbe! basi nitakuwa nimemkosea sana na kumuumiza aisee, Dah Mungu anisamehe sana kwakweli maana sikuyajua yote haya na wala sijawahi kusoma popote kujua siri hzi....Eeeh basi nadhani akawa huko bafuni na mimi nikalala,lakini baada ya muda nilikuja tu kushtuka na kusikia mlango ukigongwa na niliposhtuka nikakuta pajama yangu iko wazi na yeye amelala uchi tena,bila mpangilio (mpaka hapa mtumishi hajui kama mke wake alizimia)...basi nikawasikiliza pale mlangoni na walikuwa ni wahudumu wa hoteli na walidai kuna tatizo chumbani kwangu,lakini mimi niliwaambia hakuna shida na wao wakaondoka,basi namimi nikaenda washroom na niliporudi nikamlaza vizuri,na mara akashtuka na huku anaendelea kama kulia hivi,lakini kwa kuwa nilikuwa nimechoka sana nikajipumzisha na kuadhimia kuongea nae asubuhi,basi nikalala na ndio mpaka niliposhtuka asubuhi na kuona pajama yangu imefunguliwa tena na mke wangu hayupo na niliamshwa na simu na ndio ninyi mkaja...ila pia nilidhani labda mke wangu hapendi nywele nyingi ambazo nimefuga kichwani pamoja na huku, na kwangu mimi zilikuwa hazina shida maana zinapata matunzo lakini kwasababu ya mke wangu niliadhimia kuzinyoa pia.
 
Basi yule best akamuuliza unafugaje nywele nyingi hivyo sehemu za siri? au ndio unadhiri? anyway mpaka hapo ninapata picha ingawa bado sijui hasa nini tatizo maana mke wako hajasema kitu,jipe moyo tu kaka,naamini haya mambo yatapata ufumbuzi tu na yatafika mwisho.
 
Naam wakamalizia kupanga mizigo,nayo wakaitoa nje,wakafanya malipo na kuwaombea msamaha wale wafanyakazi na mlinzi,kama uongozi wa hoteli uliwasamehe au laa sijui,ila mimi ninachojua ni kuwa hatimaye zawadi alienda nazo mama mkwe kwa mujibu wa makubaliano na huyu kijana akaenda zake kwao Huko mkoani(naomba nisitaje mkoa) na habari za chini chini zikavuma lakini sio kivile na baada kama ya wiki mbili yule mtumishi akarudi na akawa haonekani saaana na yeye ndiye alisoma ule ujumbe wa mke wake na hakumwambia mtu maana alijua siri nzito. alijitahidi kuwakwepa watu na hata waliomfikia alijitahidi kuuma maneno na siku zikasonga kwa neema za Mungu. Baada ya miezi mitatu yule dada alirudi kwao na mama yake alifurahi mpaka akatoa machozi,hakuweza kumfokea zaidi ya kuonyesha kutokufurahia kabisa jambo hilo maana limemtia aibu mama yake,na hapo baada ya kubanwa sana akaamua kusema mkasa mzima na ni kwanini alikimbia........ITAENDELEA!!!
 
(Hapa ni muhimu kukazia sana kwamba ndoa ni makubaliano ya hiari ya watu wawili na sio msukumo wa watu wa nje kama wazazi na marafiki,kama umempenda mtu na ukaamua kwa dhati kuoana nae basi uutumie muda wa uchumba vizuri kufahamiana,sijasema kujuana kimapenzi hapana! ila kuna mengi mnaweza mkajadili na hata ukajua mtazamo,uelewa na uzoefu wa mambo mengi ya kijamii na hivyo kujua namna ya kuendana nae...na kama ukikaa vizuri na Mungu,lazima akujulishe mambo yote yaliyo sirini sawasawa na kutaka kwako kujua sawasawa na imani yako kwa Mungu na kwa kadri ya imani na nguvu ya Mungu itendayo kazi ndani yako,sop muda wa uchumba mnawaza outing,beach,movie na mnashindwa kuyatazama maisha katika upana wake....NAJUA KUNA MTU HAPA ANATAMANI KUNIRARUA,HAYA NGOJA NISIWAKWAZA HADITHI INAISHA NAMNA HII......)
 
.....MALIZIA!!!  
 Kwanza akaomba msamaha sana kwa mama yake na kwa wote kupitia mama yake na taratibu akaeleza ya moyoni mwake.....Mama ni kweli nampenda sana "X" na nilikubali kuolewa nae kwa moyo mmoja,lakini yeye anafanya kila jambo lionekane ni la kiroho na kwasababu ya ushamba mambo mengi sana hajui na ameishia kuniumiza tu siku ile ya kwanza...mmmh! (Mama akakaa kwa makini na kutega sikio,eeeh sema mwanangu)
.....Baada ya yote hayo niliyosema wala haikunisumbua sana ila wakati tunafanya,bila hata kuniandaa aliniingilia,na ukweli nilisikia maumivu sana kwa jinsi ilivyokuwa kubwa na baada ya muda mfupi alimaliza na kulala,lakini kilichonishangaza mbona hata alivyomaliza yeye,ingawa hakujali kama mimi nimefika au laa,mbona sikuona badiliko ya hiyo .....yake,basi baadae niliamua nimchungulie nijue hasa kwa undani,basi alipolala nikamfungua na kumchungulia na dah! hapo nikashutuka kuona hiyo nanii kubwa na bado imesimama na rangi yake haifanani ya mwili wake,basi hapo nilizimia na baadae nilizinduka na kuanza kulia,na kwasababu sikuamini nilichokiona,nikasema nitathibitisha tena,basi mara hii alipokuwa amelala nilifunua tena na kupapasa mkono,lakini mara hii cha kushangaza ni kuwa, ile kitu haikuwepo na hapo nilipogusa nikaona tu kakitu kadogo sana ndani ya minywele na hapo nikahisi kama naona mazingaombwe,na baadae niliona maisha haya siwezi kuishi mpaka kufa ndio nikaamua kuondoka!
 
(Najua unatamani kujua nini hasa kilikuwa pale ndani....ndio ukweli ni kuwa mtumishi yule alikuwa ana maumbile madogo sana (kidole chanda) na hivyo kwa ushauri wa marafiki wa karibu aliamua kununua Dido (artificial P.) na kuamua kuuvaa pale anapofanya bila kumwambia mkewe ukweli,na hiyo ndio iliyomgarimu sana kijana huyo....ni muhimu sana kuomba ushauri wa karibu sana kwa watu unaowaamini ikiwa mwilini mwako kuna upungufu au ulemavu,isije kuwa na wewe unajua kabisa huwezi kuzaa kisha unaoa au kuolewa na kuanza kumsumbua mwenzako kwa maombi na tabu hali unajua wapi ulijikwaa....kwa habari ya maumbile,yawe makubwa au madogo,ninaamini kuna namna unaweza kusaidiwa na madaktari na washauri kabla ya kamua kuoa au kuolewa)
 
N.B; Ninaomba mnisamehe kwa lugha ya kuumiza hisia zenu ila naamini kuna mtu kasaidika katika hadithi hii,hatuwezi kuandika kila kitu hapa ila Mungu akupe hekima ya kujifunza kila ambacho ingefaa ujifunze.
 
....KAMA YULE KIJANA ALIOA TENA AMA KUONANA NA MKE WA KE TENA MIMI SINA HAKIKA,ILA NINAJUA JAMBO MOJA TU KUWA MPAKA SASA WATU HAWA HAWAKO PAMOJA!
 
SAWASAWA NA Wafilipi 4:8...."Hatimaye ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa njema, ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote,yatafakarini hayo."
 
 MUHIMU SANA TOKA KWA MWANDISHI;
1.Sijaandika habari hii ili kukushawishi wewe kufanya sasa, ila nataka upate mwanga mkubwa zaidi kuwa mambo ya ndoa ni makubwa zaidi ya vile unavyowaza,hivyo kama unaomba Mume au Mke basi hakikisha unamwamini Mungu kwa 100%
2. Ni marufuku kujaribu kufanya,kuonyeshana hata kushika sehemu za siri za mwenzako kabla ya ndoa
3.Sitaki utumie akili yako kuikabili hofu ambayo imejengeka ndani yako baada ya habari hii ,ila nataka umwamini Mungu kuwa ukiwa mwaminifu na msikikivu Bwana atakufunulia yale yote ya sirini hata ambayo mwenza wako amekuficha.
4. Hakuna raha yoyote honeymoon kama ulishaanza kufanya mapenzi na mwenza wako huyo kabla ya ndoa, na hata wale wanaoenda honeymoon, sio lazima muanze kufanya siku hiyo hiyo mnayofika...kwa kuwa mnakuwa mmechoka na hamjuani vema hapo kitandani,basi mnashauriwa kupumzika na pale mnapoamka na kuwa na nguvu fresh,baada ya kuoga asubuhi, ndi hapo sasa mnaweza mkaanza ibaada kwa michezo na mashamushamu ya ha hapa na pale...hapo mtakuwa mnaandaa hisia zenu na kupata nafasi ya kujuana kila mmoja anafurahia zaidi nini,wapi na kwa vipi?
5. Ni marufuku kutumia hayo mapicha ya ngono kama mwalimu ndani ya ndoa,hizo picha zimechezwa kibiahsra na nyingine ni kazi ya kumpyuta,humo ndani watu hutumia madawa,na hufanya mengi kwa influence ya kipepo,sasa usije ukaaingiza tabia za kikahaba na maroho yake ndani ya ndoa yako
KUNA NAMNA YA KUFANYA NA KUFURAHIA TENDO LA NDOA NDANI YA NDOA KWA AJILI YA KILA MTU, BILA KUJALI MAUMBILE,VIMO WALA CHOCHOTE, MUHIMU NI KUKUBALI KUFUNDISHIKA NA KUWA TAYARI,VIPO VITABU VIMEANDIKWA NA WATUMISHI WA MUNGU...UKIFIKA WAKATI WAKO BASI NENDA KATAFUTE KWA BOOKSHOP,MFANO "TENDO LA NDOA" NA VINGINEVYO!!!
 
*********MWISHO (THE END)************* 

Kwa Maoni, Ushauri na Neno lolote,hata kama ni Stori ya kweli toka Mtaani kwako au Maishani mwako basi check me out!!!
+255 713 883797
@Imedhaminiwa na http://quality-love.blogspot.com
(c)2013
  

No comments:

Post a Comment