Wednesday, July 24, 2013

USIKU ULE WA KWANZA WA FUNGATE (HONEYMOON)-Part 2

kwa wale wenye kumbukumbu nzuri,nilianza kuwaletea habari moja toka huko kibaha na nilikuwa kimya kwa muda ili kupata habari kamili za yote yaliyojiri, naam kwa wale ambao hawakusoma iliyopita,ninawasahuri waanzie kwanza hapa kisha tuendelee

http://quality-love.blogspot.com/2013/06/usiku-ule-wa-kwanza-wa-fungatehoneymoon.html

.......Lakini baada ya miezi mitatu nilienda tena huko kibaha ili nijue nini kinaendelea katika sakata hilo na hapo ndio nikagundua kuwa kumbe yule kijana alikuwa..........ENDELEA Part 2

*********************************************************************************

...Mtumishi aliyetumika kanisani kwa kipindi kirefu pamoja na baba yake mzazi na binti huyu,na kijana huyu kwa jinsi alivyokuwa akijitoa na kwa namna alivyohudumu na mchungaji huyo kwa muda mrefu,alipendwa sana aitha kwa utani au kwa kumaanisha mchungaji amewahi kusema..."Nitakupa zawadi ya mke toka nyumbani kwangu" na kipindi hicho mama mzazi alisikia na aliamini hivyo, sema bahati mbaya sana Mchungaji alifariki kabla ya kushuhudia binti yake anaolewa na nani.

Kwa hakika kijana alilewa katika maadili ambayo hata mabadiliko ya sayansi na tekinolojia alikemea na kuona ni dhambi....kijana huyo hakupenda TV wala hakusoma magazeti,kwake Biblia na maombi vilitosha kabisa kujua ulimwengu unaendaje.
Bado haifahamiki kuwa kijana huyu amewahi au hajawahi kuwa na mahusiano au kufanya mapenzi hapo kabla ingawa amewahi kutengwa kwa.......(nitazungumzia hapo mbeleni).
Ila kwa taarifa za mama mzazi wa binti yule, nilizopata wakati akimfokea mwanae kwa kitendo alichokifanya ni kwamba, baada ya harusi tu wakiwa kwenye gari kwenda honeymoon Kijana huyo alianza kwa kumshikashika taratibu huku akishukuru binti huyo kuolewa na yeye,inavyoonyesha kijana huyo hakumshika kwa msukumo wa kimahaba ila kwa kupata hiyo nafasi ya kuwa nae karibu sana kwa mara ya kwanza, na kwahiyo binti joto likapanda sana na kwa kuwa alikuwa yuko na mume wake aliamini usiku ule utakuwa wa kihistoria na hii ni kwasababu ya siku ile kuwa mbaya kwake (High heat katika mzunguko wake), na kwa kuwa alikuwa hajafanya kwa muda mrefu (ikumbukwe kuwa binti huyu amewahi kukengeuka na kufanya ufuska sana kabla hajarejea kundini na hivyo uzoefu wa mtaani ulikuwa mkubwa sana) na zaidi ya yote alikuwa tayari ameanza kushikwashikwa, samahani kwa lugha ya wazi lakini nimetamani ujue ukweli wote yamkini na wewe ukakusaidia kwa namna moja ama nyingine.
Basi walipofika hapo hotelini,walishushiwa zawadi zao na wale wasimamizi wakateta nao kidogo kisha wakawaacha na kuondoka zao.

Basi walipobaki peke yao,yule binti alimrukia kijana kwa kumbato la kubembea na kisha akaanza romance,lakini kijana huyu hakuonekana kupendezwa na hilo labda kwasababu hakujua na hivyo alijitahidi kuvumilia lakini hatimaye akamshusha chini na kumwambia yaliyokuwa kichwani mwake, basi binti akakubali na kuanza kusikiliza huku joto likiwa juu vibaya mno,basi yule kijana akasema natamani tumshukuru Mungu kwanza kwa sisi kufanikiwa kufunga ndoa na tuweke mikononi mwa Mungu yoote yaliyo mbele yetu,basi wakapiga magoti kando ya kitanda (huku binti akiwa na hamu yale maombi yaishe haraka),basi kijana wa watu alianza kuomba na kushukuru,akazama na kuanza kunena sana....yule binti masikini akaona hii sio akaingia kuoga na kurudi amevaa taulu,lakini mtumishi alipomwona binti na taulo ndio akaanza kukemea mapepo masalia ya uzinzi ndani ya mke wake na kuomba sana,
Binti alipochoka kusubiri akajilaza kitandani kwa hasira na kwa sababu ya uchovu na hasira kajiusingizi kakampitia......na huku baada ya maombi ya mtumishi ya takribani masaa mawili, nae akaenda kuoga na kurudi akiwa na pajama na kumkuta mkewe amepitiwa na usingizi akiwa amelalia mgongo akiwa na Taulo tu, basi hivyohivyo Mtumishi huyo akaamua kum...........ITAENDELEA!!!

(Unaweza kuhisi mtumishi aliamua kufanya nini hivyohivyo?....usijali usikose mwendelezo wa hadithi ya kweli toka kibaha,ili ujifunze kwa faida yako!!)

@Kwa hisani kubwa ya http://quality-love.blogspot.com/ (c)2013
King Chavala-MC
+255 713 883 797

No comments:

Post a Comment