Wednesday, June 19, 2013

"USIKU ULE WA KWANZA WA FUNGATE(HONEYMOON)"

UTANGULIZI;
Mwaka jana tulikwenda harusini huko kibaha,pwani na harusi kwa hakika ilipendeza kwa jinsi kamati ilivyojiandaa,naam shughuli ilikuwa motomoto kwasababu bibi harusi alikuwa ni binti pekee wa mchungaji,ambaye alikuwa anaishi tu na mama yake baada ya mchungaji kufariki dunia ajali ya majini akitoka kuhubiri injili huko visiwani mafia...na ilikuwa ni furaha pekee ya mama maana alisemwa mno kwasababu ya binti huyo,ndio binti huyo amewahi kukengeuka na kumtumikia shetani kwa kipindi fulani kabla hajarejea kundini.

KIINI CHA STORI;
Baada ya hizo shamla shamla na shamra shamra zote kukamilika basi sisi tulirejea makwetu tukiwatakia safari njema ya kwenda huko mwezini,na walipata bahati ya kwenda hoteli moja ya heshima tu inayotosha kabisa kufikia raha ya kilele cha huko mwezini bila bugudha!

N.B; Kwa kawaida makanisani kwetu huku watu hutakiwa kupima kwanza kabla ya kuona,lakini changamoto ni kuwa imekaririwa kuwa Ukimwi peke yake ndio inaweza kuwa kikwazo cha ndoa na tunasahau kuwa kuna magonjwa mengione kama vile sickle cells,magonjwa ya moyo,strelity hata size za maumbile ni muhimu kuwa na tahadhari in case kuna abnormalities)
...Sasa taarifa zilizotufikia ni kuwa baada ya kufika huko honeymoon,yule bibi harusi alifungasha saa kumi na moja asubuhi na kupotea huku akiacha kinote mezani....HAPANA,MIMI NAONA SIWEZI,NISAMEHE!
Na akamwandikia mama yake text hii..."Mama samahani,nitakuwa salama tu usinitafute,niliolewa ili furaha ya maisha iwe na heshima kwangu,ili niliokuta huku siwezi mama,bye" Na kisha akatuma line.
Yule Bwana harusi aliamua kurejea nyumbani akishindwa kusema hasa tatizo ni nini na nini kilitokea...na hivyo kuacha gumzo mtaani kote na kila alibaki kusema analohisi na kuona linafaa mdomoni kwake,wengine wakimsema mama mzazi kuwa alilazimisha ndoa,wengine wakisema binti hajatulia na hata wengine wakimsema huyu kijana wajuavyo.

   Lakini baada ya miezi mitatu nilienda tena huko kibaha ili nijue nini kinaendelea katika sakata hilo na hapo ndio nikagundua kuwa kumbe yule kijana alikuwa............ITAENDELEA!!!!!

(Unaweza ukajaribu kukisia niligundua nini huko,lakini hayo yatakuwa ni yako ukweli nitauleta mwenyewe)

@Kwa hisani kubwa ya http://quality-love.blogspot.com (c)2013
King Chavala-MC
+255 713 883 797

2 comments: