Thursday, June 27, 2013

VITU VYA MUHIMU VYA KUANGALIA UNAPOOMBA MWEZI WA MAISHA!!!!hABARI ZENU!!!!
Watu wengi inapofika katika swala la kutafuta mwenzi wa maisha,nikiwa na maana mume au mke huwa inakuwa ngumu sana. Maana wanakuwa hawajui wafanye nini ili waweze kupata ubavu ambao ndio Mungu amekusudia na sio kuchukua ubavu wa wenzao. Ni jambo la maana sana unapotafuta au kujiandaa kuwa na mwenzi wa maisha kujua mambo muhimu yatakayo kusaidia kuepusha kukutana na mwenzi sahihi kutoka kwa Mungu.

Leo nitaelezea mambo muhimu matatu tu japo hii itakuwa series ambapo tutaendelea kueleza zaidi na zaidi juu ya vitu muhimu tunavyoendelea huko mbele.
Mambo hayo ni;
1.       Maombi
Maombi ni muhimu sana na yanakufanya uwe na ushirika na Mungu,na unapoomba ni ishara ya kumwambia Mungu kwamba bila wewe Mungu wangu siwezi. Kuna mchungaji mmoja alitufundisha ni muhimu kufanya maombi pale ambapo huna picha yoyote kichwani,maana tatizo la watu wengi ni kwamba wanakwenda kuomba Mungu huku ana picha ya mtu Fulani,au mwingine anamwambia Mungu ooh Mungu nipe huyu,nataka kukumbia rafiki hiyo sio njia nzuri.

Wewe muombe Mungu akupe mwenzi,halafu kama neno lake linavyosema kwamba tukiomba tuamini kwamba ametupatia na kwamba Mungu si dhalimu maana yeye ni baba atatupa kitu chema,basi tuamini hivyo.Ukishaomba na kuamini kwamba umepata hata kama katika hali halisi huoni anza kumshukuru Mungu kwa mwenzi mzuri kutoka kwake.

Mtumishi mwingine alifundisha unaweza kusema huyo mtu awe na haiba gani n.k,lakini ujue kwamba Mungu yuko juu ya vyote atakaye kupa ndio sahihi kuliko akili yako inavyohitaji au kudhani.

Maombi ni eneo muhimu sana ni vizuri ukawa na mtu ambaye mnaelewana na kiimani mko katika level moja au yeye amekuzidi mkawa mnaliombea hilo pamoja na mambo mengine yanayowazunguka,maana neno lake linasema palipo wawili watatu yeye yupo katikati yao,upako wa uwingi nao una umuhimu sana.

Unapukuwa katika maombi ni vizuri pia ukatubu maana unaweza ukawa na vitu vinavyozuia mawasiliano yako na Mungu. Tubu kwa chochote ambacho umefanya kwa kujua au kutojua maana Mungu wetu ni mtakatifu uende mbele zake ukiwa mweupe,Amen

2.       Je wewe ni mtu sahihi au unayefaa kuoa au kuolewa
Kitu kingine cha kuangalia nafikiri ni vizuri kujifanyia utafiti wewe mwenyewe,kujichunguza hivi kweli mimi kweli nina tabia gani ya kufaa kuishi na mtu mwingine.
 Hivi kweli mimi ninazo tabia za mke au mume mwema kweli ?
 Hivi mimi ni mtu ambaye watu wanaweza kumwamini na kumpa moyo wake kweli?

Ni kwanini nataka kuolewa au kuoa? Nataka kuolewa au kuoa  kwasababu mama au baba yangu anahitaji hivyo,au kwa vile rika langu wote wameolewa? Jamii inanionaje kwanza?
Ukijitafiti utagundua kwa njia moja au nyingine kuna mtu alishakupa mrudisho nyuma juu ya tabia zako mbaya,je kwa hizo tabia kweli bila kuzibadilisha kuna mtu anaweza kuishi na wewe? Jiulize peke yako wala usimuulize mtu,utapata majibu hayo utashangaa ambavyo unahitaji ujishughulikie kwanza. Watu wengi wanalia katika maombi oooh Mungu baba Jehova,naomba unipe mtu anayefaa kuwa mume au mke wangu lakini wao wanasahau hivi mimi Mungu ananionaje,kweli maisha yangu yanampa Mungu utukufu. Unaweza ukawa na vitabia ambavyo unaona kwamba si vibaya kumbe hivyo hivyo vyaweza kusimama kama kizingiti cha Baraka zako.
Ukishajua tatizo liko wapi badilika,saa nyingine kuna watu wanakuja na nia ya kuwa wenzi halafu wanaingia mitini basi ukijikagua unaona inawezekana tabia hii ndio imemkimbiza,basi vizuri kufanyia kazi na sio kukaa na kulia.
Kwakweli ni heri umlilie Mungu atakurehemu kuliko huyo aliyekukimbia maana akishaamua ndio ameamua na kama sio ubavu wako basi acha aende kwa ubavu wake,Amen

......TUTAENDELEA!!!! na somo hili,masomo haya yameandaliwa na Blogger wa Rejoice and Rejoice link http://rejoice-and-rejoice.blogspot.com/

Wednesday, June 19, 2013

"USIKU ULE WA KWANZA WA FUNGATE(HONEYMOON)"

UTANGULIZI;
Mwaka jana tulikwenda harusini huko kibaha,pwani na harusi kwa hakika ilipendeza kwa jinsi kamati ilivyojiandaa,naam shughuli ilikuwa motomoto kwasababu bibi harusi alikuwa ni binti pekee wa mchungaji,ambaye alikuwa anaishi tu na mama yake baada ya mchungaji kufariki dunia ajali ya majini akitoka kuhubiri injili huko visiwani mafia...na ilikuwa ni furaha pekee ya mama maana alisemwa mno kwasababu ya binti huyo,ndio binti huyo amewahi kukengeuka na kumtumikia shetani kwa kipindi fulani kabla hajarejea kundini.

KIINI CHA STORI;
Baada ya hizo shamla shamla na shamra shamra zote kukamilika basi sisi tulirejea makwetu tukiwatakia safari njema ya kwenda huko mwezini,na walipata bahati ya kwenda hoteli moja ya heshima tu inayotosha kabisa kufikia raha ya kilele cha huko mwezini bila bugudha!

N.B; Kwa kawaida makanisani kwetu huku watu hutakiwa kupima kwanza kabla ya kuona,lakini changamoto ni kuwa imekaririwa kuwa Ukimwi peke yake ndio inaweza kuwa kikwazo cha ndoa na tunasahau kuwa kuna magonjwa mengione kama vile sickle cells,magonjwa ya moyo,strelity hata size za maumbile ni muhimu kuwa na tahadhari in case kuna abnormalities)
...Sasa taarifa zilizotufikia ni kuwa baada ya kufika huko honeymoon,yule bibi harusi alifungasha saa kumi na moja asubuhi na kupotea huku akiacha kinote mezani....HAPANA,MIMI NAONA SIWEZI,NISAMEHE!
Na akamwandikia mama yake text hii..."Mama samahani,nitakuwa salama tu usinitafute,niliolewa ili furaha ya maisha iwe na heshima kwangu,ili niliokuta huku siwezi mama,bye" Na kisha akatuma line.
Yule Bwana harusi aliamua kurejea nyumbani akishindwa kusema hasa tatizo ni nini na nini kilitokea...na hivyo kuacha gumzo mtaani kote na kila alibaki kusema analohisi na kuona linafaa mdomoni kwake,wengine wakimsema mama mzazi kuwa alilazimisha ndoa,wengine wakisema binti hajatulia na hata wengine wakimsema huyu kijana wajuavyo.

   Lakini baada ya miezi mitatu nilienda tena huko kibaha ili nijue nini kinaendelea katika sakata hilo na hapo ndio nikagundua kuwa kumbe yule kijana alikuwa............ITAENDELEA!!!!!

(Unaweza ukajaribu kukisia niligundua nini huko,lakini hayo yatakuwa ni yako ukweli nitauleta mwenyewe)

@Kwa hisani kubwa ya http://quality-love.blogspot.com (c)2013
King Chavala-MC
+255 713 883 797

Monday, June 17, 2013

"29/09/2013".....OPEN LETTER TO ALL FROM KING CHAVALA!!!

MY FAITH & WISH(29/09/2013) Vs GOD'S BEST TIME OF GIVING ME A GIFT OF A WIFE....Mmmhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!?????????????????
*****************************************************
Hivi siku za karibuni nimekuwa nikipokea maswali na maulizo mengi sana,yaliyokaa katima mfumo wa uhojiji usio rasmi na kumbusho la habari ya hatma yangu ya "KUKAMILIKA"....na nimekaa kimya makusudi kwasababu kwa kadri nilivyoongea kila siku hata kama nimeongea haya ndani ya mwaka mmoja tu,watu wanaona kama niliaanza kuahidi miaka hiyoooo!
Anyway natamani niwajibuni nyote kwa pamoja kuwa VILE AMBAVYO NILISEMA,NDIO NILIMAANISHA KUMWAMINI BWANA KATIKA JAMBO HILI!.....unajua katika ulimwengu huu EVERYTHING IS DONE BY FAITH....Martin Luther King,amewahi kusema...You need not to see the whole staircase,just start the first step by faith!
***********************************************************

Pamoja na carrier yangu kama MC/Comedian,katika hili sijalifanyia utani,i was and i am very serious about it!.....But this issues need preparations na kuhusika kwa watu wengi sana,kwa mwezi wa pili mpaka wa nne tumepoteza 4 ndugu(Baba mkubwa,bibi mzaa baba,binamu na mjomba kaka wa mama) so kwa hali ya kawaida hakuna namna ningeanza process kwa hali hii,na zaidi ya hiyo in my church there are are some strictly steps and procedures to follow that are taged within 6months!
SO MY FAITH IS CONSTRAINED IN THIS NARROW PATH THOUGH I BELIEVE IN MIRACLES...The Bible says"Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu,bali jawabu la ulimi latoka kwa Bwana",so no way if at God is in Control mimi ni nani hata nibishane au nifanye tofauti ili tu kutunza promise yangu ya 29/09/2013 while God's time is the best time?
***********************************************************
Nilimwamini na bado namwamini Bwana kwa habari ya mwana-mwari asiye na kunyanzi lolote moyoni,naam nafsi yangu ikaona,lakini RIDHAA ya ayala yule haikuwa kwangu,yamkini nafsi zangu zilitafasiri vibaya ama labda sikufanya vema yaliyonipasa ama muda wake wa kupata kiuu bado mmmh! ni nani ajuaye siri za Bwana na akaenda kinyume na maagizo yake....yeye amezitukuza ahadi zake kuliko hata Jina lake,naam naamini itatimia kwangu!!
**********************************************************
NILITAMANI SANA NA BADO NATAMANI KUFANYA 29/09/2013 KAMA NILIKWISHA KUKIRI NA KUAMINI HIVYO,LAKINI IKIWA SITAPATA KIBALI CHA BWANA KWA SAA HIYO,SITAMLAUMU MUNGU HATA KIDOGO,KWA KUKWA KATIKA MAMBO YOTE YEYE HUFANYA KAZI NA WALE WAMPENDAO KATIKA KUWAPATIA MEMA!!
**********************************************************
Moyo wangu unaweza kuumia kumkosa binti yule hata sasa,lakini bado ninayo nafasi ya kuiambia nafsi yangu....PRAY FOR WHAT YOU DESERVE AND NOT WHAT YOU WANT(Maana yawezekana ukang'ang'ania kupata gari kumbe unastahili ndege,ama ukaomba treni sana kumbe unastahili kupata pikipiki....naam najua na ninaamini mke ni zawadi,Je ni nani mwenye utimamu kichwani ambaye huletewa zawadi na kabla hajaifungua akaambiwa zawadi yako sio hiyo bali ni hii na akapewa nyingine,nae akang'ang'ana kwa kusema...HAPANA MIMI NAITAKA HII,KWASABABU HII NDIO NZURI NA NIMESHAIZOEA MACHONI,hali hata hajui ndani kunani???)
Naam nimelazimika kuandika waraka huu kwenu,nyote wenye mapenzi mema na mimi na mnaniombea kheri ili msiache kuniombea kila siku maana huduma yangu ni kubwa na ni ya mataifa mengi,hivyo mke si jambo dogo wala la masikhara,hapa unamzungumzia mshauri na msaidizi wa "ICON OF AFRICA"
**********************************************************
MSINISUKUME WALA KUNISII KUOA ETI KWASABABU MARAFIKI ZANGU WENGI WAMEOA AU WANAOA,BALI MNISII NILITEGEE SHAURI LA BWANA NA KUONA KAMA YEYE AONAVYO!!!
**********************************************************
Kwa wale mliotendwa,kuachwa na kuumizwa,msione kama hapo ndio mwisho wa dunia,bali kaeni chini mjichunguze na kama kuna mahali kuna kosa basi jisahisheni na kusonga mbele,Biblia inasema.....Wakati wa Mazuri ufurahi,na wakati wa mabaya ufikiri,maana yote haya hutokea kwa kusudi!
Wakati mwingine hampati kwasababu mnang'angania mno vya zamani,au mnatafuta kwa lengo la kuwakomoa mliotendana nao,hiyo sio sawa!!
Msiache kuwapenda na kuwaombea wale waliowatenda ama hata wale wasiowapenda ninyi na huo ndio ukubwa.
********************************************************
Kwa wale mnaongoja kwa hamu harusi yangu,bado msichoke na wale wote walio kwenye michakato hivi sasa ya kuoa nawatakia kheri,hongereni kwa hatua na Mungu aimarishe mioyo yenu hasa katika kipindi hiki kisicho chepesi!
Namwamini Bwana kuwa saa ikifika basi mambo yote yatakuwa SAFIIII!
************************************************************
This are my words from my mind and my heart,if you are friend or fan or whatever,hit the "like" after reading and "share" if you wish!
I LOVE YOU AND I LOVE YOU SO MUCH!
Thank you!

Regards
King Chavala-MC
http://kingchavala.blogspot.com/