Monday, August 12, 2013

USIKU ULE WA KWANZA WA FUNGATE (HONEYMOON).........Part 4!!!Hello rafiki habari yako!
Naamini umekuwa unafuatilia sana habari hii
Iliyoanzia hapaSAWASAWA NA Wafilipi 4:8...."Hatimaye ndugu zangu, mambo yo yote yaliyo ya kweli, yo yote yaliyo ya staha, yo yote yaliyo ya haki, yo yote yaliyo safi, yo yote yenye sifa njema; ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa njema, ukiwapo wema wo wote, ikiwapo sifa nzuri yo yote,yatafakarini hayo."

NDIO NA MIMI NAWALETEA SIMULIZI HII ILI MWISHONI KWA PAMOJA TUTAFAKARI;

ILIPOISHIA PART 3;
....mara alivyofunua tu hivi na kumwacha mumewe Uchi kabisa....Binti alishtuka kwa mshangao na kusema "Mamaaaa" na hapo akaangukia kitandani na kuzimia...............

ENDELEA SASA NA PART 4; 
Na kwasababu mume wake alikuwa amepitiwa na usingizi wa kuchoka,hata uliposikika ule mshindo pamoja ile sauti ya “mamaaa”, mume wake hakusikia ila inahisika kuwa kuna watu walisikia chumba kingine na hivyo wakaamua kugiga simu mapokezi na kuwatarifu wahudumu wa Hotel, na hiyo iliwalazimu wahudumu wa Hotel kugonga vyumba kadhaa ili kujua hasa ni wapi ilikuwepo shida….na walipogonga chumba No 307, basi toka usingizini Yule mtumishi akashtuka kwa nguvu na kuona mke wake amelala uchi kabisa tena sio kulala kivile ni kama amejibwaga tu,basi akamfunika haraka na kwenda kusikia anayegonga mlango……na alipofungua akashangaa kuulizwa kuna shida gani humu mbona kuna sauti ya mshtuko imesikika huku? Basi haraka akajibu mke wangu huwa anashtuka shtuka hata akiona mende tu, sasa yamkini kuna jambo limeshtua,ila hakuna tatizo lolote lile na kama ikiwepo shida nitawapigia simu,samahani sana kwa usumbufu….basi wale wahudumu wa hotel  wakaondoka lakini kwa shingo upande, naye akafunga mlango na kurudi ndani.

Aliporejea akawa na maswali mengi sana kichwani maana hata hakujua nini kimetokea na basi alichokifanya ni kumbeba mke wake na kumlaza vizuri kitandani….na akamlaza akiwa anatazama juu,basi kabla hajamfunika alibaki kwa sekunde kadhaa akiwa anamshangaa Mungu kwa uumbaji wa mke wake….na baada ya muda akawa ameshikwa na haja ndogo basi akakimbia mara moja chooni, na alipofika huko kwanza akashtuka sana kuwa ile pajama yake ilikuwa wazi, I mean ilikuwa imefungunguliwa na hapo akapata kigugumizi cha kuwaza…ina maana na wale wahudumu wawili wa hoteli walimuona utupu wake? Lakini hakufungua mlango wote wa chumbani mmmh yamkini hawajaona kitu….na alipotaka kukojoa akagundua kuna upungufu Fulani anao,basi akamaliza haraka na kunawa mikono na kurudi haraka na kuanza kuangalia huku na kule na kumbe ilikuwa chini ya kitanda na ilianguka pale alipostuka kwa nguvu wakati mlango wa chumba cha hoteli kikigongwa na hapo akaokota na kuweka kwenye droo ya kitanda chake, na hapo akawaza zaidi ina maana mke wangu ameona?

Basi akiwa na mikono mibichi akawa amemshika usoni kwa namna ya kumfuta machozi na kupitisha mikono mwilini mwake kwa namna ya kubembeleza na muda wote huo asijue ya kuwa mke wake amezimia na hapo akidhani mke wake amelala…..kwasababu ya ubaridi wa mikono ile na Uwezo wa Mungu tu Yule binti akashtuka na kuanza kulia….Jamani hivyo ndio nini? Maana yake nini sasa? Sitaki….sitaki……sitaki…… na kuendelea kulia kwa huzuni, basi huyu mtumishi akashangaa na kuendelea kumbembeleza jamani basi yanazungumzika…..kwa akili ya kawaida Yule mtumishi alidhani mke wake analalamikia Afro ambayo alikuwa nayo kichwani pamoja na ikulu,tena zote zilikuwa zimesheheni na zilikuwa zimetunzwa vizuri….kwa haraka unaweza ukasema labda ni nadhiri ya Bwana ya utumishi kama ya Samson, kwamba asinyoe mpaka hapo kusudi la Bwana litakalotimilika.

Yule dada akanyamaza bila kuongea zaidi nae akawa amekaa pale kitandani kwa kuwaza san asana na mume wake alikuwa ameshalala zamani sana,yaani ule usingizi wa pono, basi Yule dada akaamka na kukaa kitandani asijue afanye nini….Je aombe? Je awaambie wasimamizi wa ndoa? Au amtaarifu mama yake?....Basi akajiambia moyoni ngoja nione tena ili athibitishe kuwa alikuwa anaota au laah!
Basi taratibu akaifungua tena ile kamba ya pajama ya mume wake na kufunua taratibu, na saa alichokiona ni tofauti….”Mmmmmh!” aliguna kwa mshtuko na hapo akapata ujasiri akaingiza mkono na kupapasa,na hapo alibaki ameduwaa na hapo akawa na maswali mengi zaidi ya majibu…..mbona alichokiona hapo kwanza hakifanani na hiki,au hii ndio miujiza ya mtumishi wa Bwana,oooh hapana hakuweza kuvumilia,akamfunika bila kufunga vile kamba ilivyokuwa,akaamka na kuoga haraka na kuvaa jinsi yake na tisheti na kuchukua simu yake,pochi na vile vitu vyake vya muhimu tu na kuacha vingine vyote hapo ndani kama vile shela ya harusi na zawadi zote alizokuwa ameletewa…..na hapo akaandika ujumbe kwa mume wake na kuacha mezani na kuandika ujumbe wa simu kwa mama na wasimamizi wa harusi na kisha akaitoa ile kadi ya simu na kuitumbukiza chooni,ili asiwepo mtu wa kumtafuta…na hapo akabeba kijibegi chake, na kufungua mlango taratibu na kufanya manuva pale mapokezi na getini kwa mlinzi na kuishia zake na hiyo ilikuwa mida ya saa kumi na moja na robo.


Huku nyuma mida ya saa kumi na mbili hivi huyu jamaa alishtuliwa simu zikiita mfululizo na alipoamka cha kwanza ni kuona mke hayupo na hivyo akaenda kuangalia chooni na bafuni, holaa…chini ya kitanda holaaa…basi katika hali ya kuchanganyikiwa akatoka na pajama mpaka mapokezi na wao wakasema hawajamuona mke wake hapo,ila kuna mkaka mmoja tu ametoka alikuwa anawahi safari yake, wasijue ya kuwa binti Yule alifungua mlango mmoja ulikuwa wazi wa chumba alichokuwapo kaka mmoja akiwa hoi amelala kama amekufa na kuchukua ufunguo wa hapo na kuwasilisha mapokezi na hawa wa mapokezi sababu ya usingizi na wao walisema uweke tu hapo mezani…….hivyo Yule mtumishi akachoka na kurudi chumbani kwake haraka,akiwaacha wahudumu wa hoteli pamoja na mlinzi wakizozana na meneja maana wamekuwa wazembe…..

Yule mtumishi aliporejea chumbani akaona simu yake ina miito mikoso (missed calls) zaidi ya hamsini toka kwa mama wa binti,wasimamizi wa harusi,wazazi wake pamoja na marafiki zake wa karibu waliotaka kujua kulikoni maana wengine waliifahamu siri, basi akiwa hajakaa sawa akaona kijikaratasi mezani na anapokifuata ili ajue kimeandikwa nini,mara mlango ukafunguliwa haraka na hapo wakaingia wasimamizi wa harusi yao pamoja na mzazi wa binti akifuata nyuma na hivyo akakichukua kile kikaratasi na kuficha katika mfuko wa pajama na kukaa kitandani kwa kuhamaki,asijue awajibu nini watu hawa wenye maswali mengi yaliyojaa hofu ambayo hata yeye mwenye we hana majibu yake……Basi wakiwa wanatmbea huku na huku na kuuliza swali hili na lile, mama mkwe alibaki tu akilia pembeni kwa huzuni.

Huku chini nako mzozo ulizidi na wale wahudumu wa hoteli wa zamu pamoja na mlinzi kazi ikaota manyasi, na hapo meneja akaja chumbani na kuanza kuomba radhi kwa yote yaliyotokea,alifanya hivyo kulinda hadhi ya hoteli yao na kulinda kibarua chake,lakini mle chumbani kila mmoja alikuwa na lake na sijui hata kama walikuwa wanamuelewa….basi kwa pamoja wote wakamwambia Usijali,ahsante kama tutahitaji ushahidi wowote ule tutakutaarifu,basi meneja akatoka na kuwaacha na wao wakabaki na kuongea kitumishi na kiutu uzima na baada ya mazungumzo ya kina kiasi,basi wote kwa pamoja wakaamua ku……………………………….ITAENDELEA!!!


(Usijaribu kutabiri watu hawa waliamua nini,maana hutajua mpaka nimekujuza. Naam…..Unataka kujua Binti huyo alienda wapi? Alionekana baada ya muda gani? Na alifanya nini aliporudi? Je unajua aliona nini na yeye kudhani ni mazingaombwe? Je nini hasa ukweli wa kile alichokiona na kuamua kuikimbia ndoa yake? Je kijana alifanya nini baada ya hapo? Kanisani alionekanaje? Kwa haya pamoja na USHAURI WA MWANDISHI sawasawa na Maandiko basi….Usikose sehemu ya 5 na ya mwisho ya hadithi hii yenye ukweli na mafunzo ndani yake, kwako wewe ambaye hujakutwa na dhahama ya namna hii, Ahsante kwa kufuatilia USIKU WA KWANZA WA FUNGATE!!

INALETWA KWENU NA;
KING CHAVALA-MC
+255 713 883 797
(c)2013

No comments:

Post a Comment