Monday, August 5, 2013

USIKU ULE WA KWANZA WA FUNGATE (HONEYMOON)- Part 3

Habari zenu ndugu wasomaji na wafuatiliaji wa Mkasa huu uliotokea mkoani Pwani,pale kibaha ambapo binti mmoja alimtoroka mume wake baada ya usiku mmoja tu wa honeymoon.

Tuliazia hapa...http://quality-love.blogspot.com/2013/06/usiku-ule-wa-kwanza-wa-fungatehoneymoon.html
 
habari zenu naamini mko wazima sana, na naamini bado unafuatilia habari hii ya binti huyu aliyetoroka usiku ule wa kwanza wa fungate....habari iwe chachu kwako kujifunza na kuzingatia mambo yale ambayo yamkini huyajui lakini yamewagharimu wenzako wengi na hata sasa ndoa zao zina shida....KARIBU SANA!!
 
ILIVYOISHIA Part 2. 
http://quality-love.blogspot.com/2013/07/usiku-ule-wa-kwanza-wa-fungate.html

.....na huku baada ya maombi ya mtumishi ya takribani masaa mawili, nae akaenda kuoga na kurudi akiwa na pajama na kumkuta mkewe amepitiwa na usingizi akiwa amelalia mgongo akiwa na Taulo tu, basi hivyohivyo Mtumishi huyo akaamua kum...........INAENDELEA HAPA CHINI!

NAJUA KILA MMOJA ALIKUWA NA HISIA NA MTAZAMO WAKE JUU YA WATU HAWA, BAADA YA KUJUA KWA SEHEMU KILE KILICHOTOKEA USIKU ULE...HAMNA UBAYA YALE YALIKUWA YAKO...ILA UKWELI MWENYEWE NI HUU.....ENDELEA!!

.....shtua kwa kumtikisa kidogo, huku akimwangalia kwa macho ambayo hata yeye mwenyewe alishindwa kuyaelezea; sijui ni macho ya huruma au kuombwa kuonewa huruma,sijui ni wivu au hasira au ndio macho ya mtumishi ya kuomba msamaha...basi yule mke alivyostuka kwa nguvu toka usingizini, akajigeuza kwa haraka na taulo lake likafunguka,hivyo akabaki kama alivyozaliwa....basi huyu kijana alibaki ameduwaa kana kwamba hajui kinachoendelea....akiwa mdomo wazi kwa takribani dakika moja na nusu hivi basi yule mrembo akawa macho kabisa na akawa nae anamshangaa mbona mume wake anamshangaa kana kwamba haamini ni yeye.

    Lazima ikumbukwe kuwa kijana huyu hajawahi kabisa kujihusisha na mambo ya mapenzi zaidi ya zamani zile za utoto wakati akidimba (Hii inadhihirishwa na matendo yake ya wazi kabisa ambayo hayategemewi kutokea Honeymoon)...lakini binti ana utalaamu wa kina kupita maelezo ya kawaida,maana ameshawahi kuruka ruka huko na kisha akarejea kundini, namaanisha akarudi wokovuni na ndio hapo akapata bahati ya kuolewa.

    Basi yule binti alipoona mume wake anamshangaa akaamka na kumvuta mkono kwa nguvu,hivyo yule jamaa akaangukia kifuani kwa mke wake, na hapo mke akamkaba shingo na kumparamia kana kwamba anapanda mti lakini mti ulioinama na hapo binti akawa anajaribu sarakasi zake za mahaba...lakini kijana hakuonekana na ushirikiano saaana japo alikuwa anaweza kujigeuza na kurudia maneno yale yale zaidi ya mara ishirini...."Unajua nakupenda sana Mke wangu"...basi kwa kuwa binti alikuwa na hasira hapo kwanza, nazo zikaisha zote...na mara baada ya binti kumuelekeza mumewe kuwa naomba nishike hapa na hapa, japo kwa woga na mshangao mtumishi akafanya hivyo...japo alibahatisha tu, inaonekana ile injini ya yule mwanamke ilikuwa "ON" na ilikuwa mtelemkoni, yaani alikuwa anasubiriwa mtu tu atoe kigogo uone linavyowaka.

(Samahani kwa lugha hii ngumu, na kama itakuwa kwazo kwa yeyote tusameheane ingawa naamini kila anayesoma hapa  ni mtu mzima na anaweza kuwa anaelewa....kimsingi ashiki ya kufanya mapenzi huanzia kichwani, kama kuna ule utayari na hamu basi ashiki hiyo hupandisha joto la hisia kwa haraka sana...na wakati wa tendo, wanaume hufika mwisho wa hatua moja na kuridhika ndani hata ya dk moja mpaka tano tu, lakini kwa wanawake inaweza kuwa mara tano zaidi ya wanaume...kwa hiyo kuna maandalizi yanapaswa kufanyika ili angalau safari ianzie mahali ambapo wote wawili hawatachelewa kufika. Na kama hawa wawili wakifika kwa pamoja basi jambo hili huwa ni jema sana kwa wote)

    Basi mara tu ya yule jamaa kukumbuka kuwa yeye ni mume wa mtu na kuna kitu anapaswa kufanya, alijigeuza haraka na sasa mwanamke akawa chini na yeye akawa juu...bila kujali mwanamke anaendelea na juhudi gani, na yeye akafungua kamba ya pajama yake na kutafuta mkao wa magoti vizuri, bila kusema neno lolote, kwa pupa na kwa haraka mtumishi  "AkaINGIA"....Na basi kwa sauti ya kulalamika yule dada akashtuka na akalia kiana akisema (Akataja jina) mbona hivyo jamani?...ni dhahiri kuwa alikuwa mtulivu kwa zaidi ya miaka miwili na saa hiyo ukavu ulikuwa upo wa kutosha na ndio maana alilalamika mmh...

     Ndoa ni uvumilivu, basi yule binti akajiachilia na kuchukulia ize na akaona sio sawa kumlalamikia mtumishi wa bwana, maana kwanza hana hakika kama anajua au laah! Basi yule mdada akiwa amemwachia mumewe aendelee na ibaada, huku akawa anafanya juhudi binafsi ili angalau akaribie, basi yule kijana alijisukuma kama mara kadhaa tu,haisemekani wala kuaminika kuwa ilipitiliza mara kumi, kijana akawa ameshamaliza ibaada na kutoa matoleo na kuganda kimya kwa muda kama zile zile video za You-tube zinavyogandaga kwa internet yenye kasi ya chini....hapo kijana alikuwa amekakamaa kama vile kuna kitu kinachofolewa mwilini mwake, lakini kama ujuavyo uzoefu mpya lazima mtumishi atokwe na jasho.

     Jambo la kushangaza, baada ya yeye kutoa matoleo, akafikiri na mkewe na ibaada ishaisha kumbe masikini ya mkewe iko taratibu na ndio kwanza ilikuwa inaanza kuchanganya, ikavurugwa na wakati inataka kurudi kwenye mwendo ule wa kawaida kurudi rahani, basi yule mtumishi Akachomoka na kujifuta kidogo na Taulo na kumfuta mkewe na kisha akafunga pajama yake na kulala kando ya mkewe...yule binti alibaki kushangaa tu....hasira za uchungu zikaanza kuja na hapo mrembo yuko ile heat ya juu kabisa, basi akamwambia mumewe azime taa ili angalau ajisaidie na kusogeza mbele ibaada japo mpaka wakati wa matoleo...mume akagoma akasema hapana tuiache tu....basi yule msicha akaamua kwenda bafuni na huko akajifungia na kuamua kujisogeza manualy mpaka akafika, japo ni dhambi na sio nzuri kihivyo, lakini anasema alifika.

    Alipomaliza akakaa sana huko bafuni na kulia sana, akijaribu kufikiri hivi kweli mume wangu ndio huyu na hii ni siku ya kwanza tu yuko hivi...maisha kweli yataenda....basi mawazo mengi yakawa yanazunguka kichwani....anakumbuka nasaha wakati wa kitchen party...anakumbuka mahosia ya baba na mama...tena anakumbuka ndugu na jamaa waliowahi kuvunjs ndoa...anajaribu kukumbuka mapenzi aliyowahi kufanya huko duniani na akichanganya na wale waliowahi kumtenda....basi anataka kufanya maamuzi magumu...lakini tena anakumbuka mahubiri na mafundisho ya ndoa aliyopitia....ndio ni mpaka kifo kitakapowatenganisha.

   Basi baada ya muda akawa amepata nguvu na ujasiri na akaadhimia na yeye kwenda kumshurutisha tena mumewe ili warudie tena na hiyo ilikuwa mida ya saa tisa usiku...Basi akatoka bafuni akiwa na taulo lake na hapo akamkuta muwewe amelalia mgongo na usingizi umeshamchukua...nae akajiambia nafsini mwake nitafungua pajama hii na kufanya kila juhudi na akiamka tu nakaa juu (Ikumbukwe kuwa  mpaka hapo Msichana huyu alikuwa hajaona sehemuza siri za mumewe, maana walipofika hotelini walioga tofauti tofauti, na hata mkaka alivyompandia mkewe,yule mdada alikuwa amelalia mgongo, hivyo hakuona kitu zaidi ya kuhisi tu)

    Basi yule mwanamke akavua taulo lake na kuweka kando, naam akabaki kama alivyozaliwa...na taratibu kabisa akamsogelea mumewe na kuanza kufungua ile kamba ya pajama taratibu, na alipoifungua akaanza kuivua/kuifunua hapo akiwa na macho ya hamu na woga, anagalau aone miliki yake laivu kwa macho yake, mara alivyofunua tu hivi na kumwacha mumewe Uchi kabisa....Binti alishtuka kwa mshangao na kusema "Mamaaaa" na hapo akaangukia kitandani na kuzimia......................ITAENDELEA!!!!


(Nini alichokiona mpaka ashtuke na kuzimia? Je nini kiliendelea baada ya hapo?...Usikose kufuatilia sehemu ya 4 ya ushuhuda huu wenye kukusaidia wewe msomaji kama utazingatia kwa makini)


@Kwa hisani kubwa ya http://quality-love.blogspot.com/ (c)2013
King Chavala-MC
+255 713 883 797

No comments:

Post a Comment