******************************
Hivi siku za karibuni nimekuwa nikipokea maswali na maulizo mengi sana,yaliyokaa katima mfumo wa uhojiji usio rasmi na kumbusho la habari ya hatma yangu ya "KUKAMILIKA"....na nimekaa kimya makusudi kwasababu kwa kadri nilivyoongea kila siku hata kama nimeongea haya ndani ya mwaka mmoja tu,watu wanaona kama niliaanza kuahidi miaka hiyoooo!
Anyway natamani niwajibuni nyote kwa pamoja kuwa VILE AMBAVYO NILISEMA,NDIO NILIMAANISHA KUMWAMINI BWANA KATIKA JAMBO HILI!.....unajua katika ulimwengu huu EVERYTHING IS DONE BY FAITH....Martin Luther King,amewahi kusema...You need not to see the whole staircase,just start the first step by faith!
******************************
Pamoja na carrier yangu kama MC/Comedian,katika hili sijalifanyia utani,i was and i am very serious about it!.....But this issues need preparations na kuhusika kwa watu wengi sana,kwa mwezi wa pili mpaka wa nne tumepoteza 4 ndugu(Baba mkubwa,bibi mzaa baba,binamu na mjomba kaka wa mama) so kwa hali ya kawaida hakuna namna ningeanza process kwa hali hii,na zaidi ya hiyo in my church there are are some strictly steps and procedures to follow that are taged within 6months!
SO MY FAITH IS CONSTRAINED IN THIS NARROW PATH THOUGH I BELIEVE IN MIRACLES...The Bible says"Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu,bali jawabu la ulimi latoka kwa Bwana",so no way if at God is in Control mimi ni nani hata nibishane au nifanye tofauti ili tu kutunza promise yangu ya 29/09/2013 while God's time is the best time?
******************************
Nilimwamini na bado namwamini Bwana kwa habari ya mwana-mwari asiye na kunyanzi lolote moyoni,naam nafsi yangu ikaona,lakini RIDHAA ya ayala yule haikuwa kwangu,yamkini nafsi zangu zilitafasiri vibaya ama labda sikufanya vema yaliyonipasa ama muda wake wa kupata kiuu bado mmmh! ni nani ajuaye siri za Bwana na akaenda kinyume na maagizo yake....yeye amezitukuza ahadi zake kuliko hata Jina lake,naam naamini itatimia kwangu!!
******************************
NILITAMANI SANA NA BADO NATAMANI KUFANYA 29/09/2013 KAMA NILIKWISHA KUKIRI NA KUAMINI HIVYO,LAKINI IKIWA SITAPATA KIBALI CHA BWANA KWA SAA HIYO,SITAMLAUMU MUNGU HATA KIDOGO,KWA KUKWA KATIKA MAMBO YOTE YEYE HUFANYA KAZI NA WALE WAMPENDAO KATIKA KUWAPATIA MEMA!!
******************************
Moyo wangu unaweza kuumia kumkosa binti yule hata sasa,lakini bado ninayo nafasi ya kuiambia nafsi yangu....PRAY FOR WHAT YOU DESERVE AND NOT WHAT YOU WANT(Maana yawezekana ukang'ang'ania kupata gari kumbe unastahili ndege,ama ukaomba treni sana kumbe unastahili kupata pikipiki....naam najua na ninaamini mke ni zawadi,Je ni nani mwenye utimamu kichwani ambaye huletewa zawadi na kabla hajaifungua akaambiwa zawadi yako sio hiyo bali ni hii na akapewa nyingine,nae akang'ang'ana kwa kusema...HAPANA MIMI NAITAKA HII,KWASABABU HII NDIO NZURI NA NIMESHAIZOEA MACHONI,hali hata hajui ndani kunani???)
Naam nimelazimika kuandika waraka huu kwenu,nyote wenye mapenzi mema na mimi na mnaniombea kheri ili msiache kuniombea kila siku maana huduma yangu ni kubwa na ni ya mataifa mengi,hivyo mke si jambo dogo wala la masikhara,hapa unamzungumzia mshauri na msaidizi wa "ICON OF AFRICA"
******************************
MSINISUKUME WALA KUNISII KUOA ETI KWASABABU MARAFIKI ZANGU WENGI WAMEOA AU WANAOA,BALI MNISII NILITEGEE SHAURI LA BWANA NA KUONA KAMA YEYE AONAVYO!!!
******************************
Kwa wale mliotendwa,kuachwa na kuumizwa,msione kama hapo ndio mwisho wa dunia,bali kaeni chini mjichunguze na kama kuna mahali kuna kosa basi jisahisheni na kusonga mbele,Biblia inasema.....Wakati wa Mazuri ufurahi,na wakati wa mabaya ufikiri,maana yote haya hutokea kwa kusudi!
Wakati mwingine hampati kwasababu mnang'angania mno vya zamani,au mnatafuta kwa lengo la kuwakomoa mliotendana nao,hiyo sio sawa!!
Msiache kuwapenda na kuwaombea wale waliowatenda ama hata wale wasiowapenda ninyi na huo ndio ukubwa.
******************************
Kwa wale mnaongoja kwa hamu harusi yangu,bado msichoke na wale wote walio kwenye michakato hivi sasa ya kuoa nawatakia kheri,hongereni kwa hatua na Mungu aimarishe mioyo yenu hasa katika kipindi hiki kisicho chepesi!
Namwamini Bwana kuwa saa ikifika basi mambo yote yatakuwa SAFIIII!
******************************
This are my words from my mind and my heart,if you are friend or fan or whatever,hit the "like" after reading and "share" if you wish!
I LOVE YOU AND I LOVE YOU SO MUCH!
Thank you!
Regards
King Chavala-MC
http://
No comments:
Post a Comment