Tuesday, May 7, 2013

VIWANGO BORA VYA UZURI!!

 JE UPI NI UZURI UPITAO VIWANGO???

Hello wapenzi wasomaji,habari zenu??
Ni muda kidogo nilikuwa kimya na sio kwa bahati mbaya bali nilikuwa mapumzikoni na katika mapumziko hayo nimekuwa na muda wa kujifunza mengi na bila shaka nitaanza kuwapakulia muda si mrefu!!
Natumai kila mmoja yuko sawa na hata wale wenye changamoto kadhaa za kiafya ama kimaisha au kiuchumi ziko mwishoni kukoma maana hakuna matatizo ya kudumu wala majibu yenye umilele zaidi ya milele yenyewe.


Kwa miezi kadhaa na zaidi Leo nimekuwa najiuliza maswali mengi kuhusu UZURI!
Kwani uzuri ni nini?
Ni nani mzuri kuliko mwingine?
Je nani anaweza kupima uzuri? Kwa kipimio kipi?
Mimi najua kuwa watu wote wameubwa na Mungu na hivyo kwa Mungu hakuna mtu mbaya wala mzuri,ila kuna watu wa Mungu na Wana wa Mungu,ambao kimsingi hao wana faida nyingi zaidi na upendeleo zaidi ya watu wa Mungu!

Na uzuri wa kitu/mtu uko machoni kwa aonae hivyo,maana kizuri chako kinaweza kisiwe kizuri kwako hata kidogo na kibaya kwako kinaweza kumchanganya kabisa mwingine kwa uzuri wake!!
Hukumu ama maamuzi ya uzuri wa kitu yanayofanywa na mtu hutegemea sana na habari zilizoujaza moyo ama nafsi yake….kwa mfano,kama mtu amekuwa na watu weupe na wakamtesa ma kumkwaza hapo kale,basi hata iwaje hawezi kusifia mtu mweupe kirahisi kwasababu tuya ile kumbukumbu,lakini kama amekuwa akipata sifa njema za watu wa aina Fulani nae akazama kabisa huko basi siku ikitokea akakutana na mtu wa hulka zile ambazo alijifunza hapo kale basi lazima atampenda sana,lakini pia mtu anaweza kumpenda mtu kutokana na matamanio aliyojijengea katika maisha yake,yamkini imekuwa ni ndoto yake mtu kumpata mtu mweupe,mwembaba na mrefu basi hapo hutamwambia kitu!!

Lakini katika maisha yetu ya kila siku kuna watu ambao wana uzuri wa kusifiwa na kila mtu,na hawa ni wachache na hao tunasema wana nyota ya uzuri au GENERAL BEAUTY PUBLIC CUSTOMIZATION,na hata ukisoma katika Biblia utaona hadithi za watu wachache ambao Biblia inawataja kuwa walikuwa wazuri mfano ni Daudi pamoja na Yusufu,Yule ambae alimtega hata mke wa Potifa!

Lakini hayo yote ni ubatili,ila hizi zifuatazo ndio sifa za UZURI UPITAO VIWANGO VYA KIDUNIA!!
Ukiwa mwana wa Mungu na sio kuwa mtu wa Mungu hapo umepiga hatua ya kwanza>>>>>Na hapo ukajitambua,namaanisha ukajielewa vema KUSUDI LAKO hapo umepiga hatua ya pili>>>>Kisha ukiwa na TABIA NJEMA(CHARACTER),Basi hapo utakuwa umepanda kiwango kingine juu,unajua KIPAJI kinaweza kumfikisha mtu JUU SANA,ila ni tabia tu ndio inaweza kumfanya abaki hapo juu alipofika….Biblia inataja uzuri kwa njia hii MWEMA WA MOYO na sio UZURI WA SURA!!......Basi viwango vya juu zaidi ni kuwa MCHA MUNGU,Maana Biblia inasema….”Uzuri na upendeleo ni ubatili bali mwanamke mcha-Mungu ndie atakaesifiwa”


BASI UKIFIKA HAPO NDIO UNAKUWA NA UZURI UPITAO VIWANGO, NA SIO JUHUDI ZA KUJIKWATUA SURA NA KUKAZANA KUTAFUTA NGUO ZA KUFANANA NA HELENI,VIATU NA VIATU,NA MTU AKIWA SHAHADA NA KUPATA KAZI MAHALI BASI TENA,MKONONI AKIWA NA BLACKBERRY NA KIJIGARI KIDOGO BASI ANAJIONA MZURI MPAKA BAADAE!!

NINAWASIHI SANA,VIJANA(MABINTI NA VIJANA WA KIUME) KUJITAHIDI KUFIKIA VIWANGO VYA JUU VYA UZURI…….Youth is Glorious but is Not a Carrier!!!
BASI NIWATAKIENI UZURI MWEMA!!!

King Chavala +255 713 883 797

No comments:

Post a Comment