Thursday, July 18, 2013

#KATIKA KUTAFUTA MWENZA#....USITAFUTE ANAYEKUFAA, BALI JITAFUTE WEWE UNAPOFAA!!!!


Habari!
Ninaamini ninaongea na mtu mzima na timamu wa akili kabisa kichwani!
Ninakushukuru hata kwa kutenga muda wako wa kujifunza kwa kusoma hapa yamkini na huko kwingineko!!
Kila jambo chini ya jua lina KANUNI zake,na kanuni hizo zikifuatwa vema huwa tunatarajia matokeo mazuri lakini kama zikikiukwa basi madhara hayaepukiki!

Na kwa kuwa sisi tumezaliwa tukiwa hatujui kitu,imetupasa kujifunza kila kitu kwa kina illi tusivunje kanuni.

Sasa ambacho huwa kinanishangaza  ni kuwa yale mambo madogo madogo ambayo hayasumbui sana maishani huwa tunatumia juhudi kubwa sana kujifunza na kisha yanayogusa kabisa mioyo yetu tunafanya kimazoea na ndio maana wengi wanaumia,maana huwa tunajiamini na kufanya kana kwamba tunajua hali hatujui....na mbaya zaidi ni kuwa hatujui na hatujui kuwa hatujui....na kama haitoshi mtu anaweza kuwa na Doctrate degree lakini bado hapa akachemka na yule msukuma mkokoteni akaukata kwa kufurahia maisha yake safi ya mahusiano.

ZINGATIA SHULE HII;

1. ASIYEJUA ALIKOTOKA HAWEZI KUJUA ANAKOKWENDA
(Yaani asiyejijua yeye mwenyewe vema,hawezi kujua maishani mwake anahitaji nini hasa)

2.ASIYEJUA AENDAKO HUWA HAPOTEI NJIA
(Anayetafuta kwa nguvu ya macho huwa haridhiki na hataacha kutafuta)

Elimu yetu imetufundisha mambo mengi lakini imetuharibu mitazamo....yaani kila mmoja anajiona yeye yuko sahihi ila mwingine yeyote yule hayuko sana na tumeandaliwa kujifunza juu ya vitu vingine tu zaidi ya sisi wenyewe na tena kuvichunguza sana kwa bidii mno kabla ya kuvifanyia maamuzi.

Ndio maana mara zote watu huwa hawazingatii kujifahamu vema,kujijua tabia zao kwa kina,kuyajua madhaifu yako na hata kujifunza kurekebishika taratibu maana inawezekana....tunabaki kutafuta huyu na yule na kazi yetu inakuwa ni kukosoa tu tabia za wengine na kusahau kuwa kuna mengine wao hufanya kama kujikinga tu kwa zile tabia zao.

MFANO;
Inawezekana sana lakini ni ngumu mno kwa mtu mwenye TABIA KUU kuhusiana na mtu mwenye TABIA KUU  kama yeye i.e Mtu muongeaji sana hawezi kukaa kwa salama na muongeaji mwingine,mtu anayependa kutuma ama kuamrisha hawezi kukaa na mtu kama yeye,hivyo ni vema mtu wa TABIA KUU akawa na Mtu wa TABIA SAWIA.

Lakini jambo la msingi sana ambalo linapaswa kuzingatiwa ni hili;
USIHANGAIKE KUTAFUTA NANI ANAKUFAA,BALI JITAMBUE NA UJIFAHAMU VEMA NA HAPO UTAJUA KWA HAKIKA WAPI UNAFAA...Maana yamkini kila unayemtaka ni TOO GOOD FOR YOU!!! ama wewe YOU ARE TOO GOOD for HIM/HER!
Sasa nafikiri ubadilishe hata namna ya utafutaji wako na uombaji wako,vinginevyo utaangukia pua

UHALISIA; Unajua kuna watu wamerukaruka weeeee halafu sasa anamtaka mtu BIKIRA(Wa kiume au wa Kike)....why Mungu akupe wewe na asimpe anayemstahili?
Na wengine wako rafu rafu tu,lakini wanataka kuhusiana na watu walio smart sana,hapana haiwezekani umeshindwa kujitunza wewe mwenyewe na kisha leo Mungu akupe treasure yake ili nayo uichakaze....Ni kweli Mungu anatupenda sana na anatuwazia mema mno lakini hawezi akaruhuru Mtoto mchanga aendeshe Hammer maana itamuua tu japo mtoto anatamani aendeshe kama wakubwa!!

HIVYO MARAFIKI NINAWSIHI SANA USILAZIMISHE URAFIKI WALA MAHUSIANO KWASABABU TU UNAMTAKA YULE AMA HUYU,LAKINI ACHA KUWA NA MAAMUZI HURU NDANI YA NAFSI YA KILA MMOJA NA HAPO NDIO MTADUMU,VINGINEVYO UNAWEZA KWENDA DUKANI KUNUNUA NATI KWA KUBAHATISHA TU,LAKINI LAITI UKIJUA BOLTI YAKO NI SAIZI NGAPI NI RAHISI KUTAFUTA NATI HUSIKA PAMOJA SPANA YA KUKAZIA!!!

AHSANTENI

King Chavala-MC
+255 713 883 797

No comments:

Post a Comment