Monday, September 2, 2013

TERABYTE LOVE (UPENDO BABKUBWA)......Part 1

Always Quality love is for Quality people!
UTANGULIZI;
......Ninakuletea cha kijana mmoja msomi mwenye shahada mbili alizozipata ughaibuni, mtaalamu ya falsafa, mtoto wa Mtumishi mkubwa wa Mungu mwenye heshima ya pekee katika jamii,Askofu wa Pentekosti ambaye pamoja na upinzani na maroroso yooote ya jamii yake alimpenda na kuamua kumuoa Dada mmoja fundi cherehani, mlutheri aliyedharaulika na ni mlemavu wa ngozi (Albino) na hata sasa wanaishi pamoja kwa furaha....unajua ilitokeaje tokeaje? Basi ungana nami taratibu tujifunze kupitia hadithi hii!
.............SIJAWAHI ONA UPENDO KAMA HUUUUUUU!

ENDELEA SASA.....
Katika maisha yangu ya pita pita hapa na pale nilikutana na jambo ambalo lilinishtua kibinadamu maana sio kawaida na nikatamani kupuuzia na nikaenda zangu,lakini nilipoondoka niliendelea kujiuliza hivi kwanini sikufuatilia kwa kina? basi tena siku zikaenda na jambo lenyewe likawa limepotea kichwani kama vile tamthilia inavyokwisha.

Basi nikajifariji ya kuwa ni jambo la kawaida tu na yamkini ni hisia zangu tu au ni maneno ya watu katika huo mtaa, maana watu nao wana visa hatari aisee!
Basi siku zimeenda na sasa imepita miaka mitatu, nikiwa nimemsindikiza mwenyeji wangu hospitali maana alijikata na bati wakati akitengeneza banda la mbwa wake, baada tu ya kupaki gari kwa mbali nikamuona kama ni mtu ninayemfahamu kwa mbali, lakini nikajiambia anyway yamkini nimechanganya tu habari, basi tukaingia hospitali na huyo ndugu yangu akasafishwa na kushwonwa na hatimaye kufungwa na pamba vema kabisa.....sasa wakati huyo ndugu yangu anasubiri kuingia theatre ili akashonwe maana palikuwa ni pakubwa sana, basi mimi niliamua kujipa tour ndani ya ile hospitali kubwa ya mkoa, ili nione ni kwa namna gani imejengwa na kupangiliwa, basi nikapiga mizunguko ya kutosha, niliporudi kwa rafiki yangu, nikakuta bado hajatoka, ndio hapo nikajiambia ngoja nikatishe kwenye moja ya mawodi, basi wakati napitta hivi mara nikamuona Dada, kimsingi ni mama kwasababu alikuwa amejifungua watoto wanne kwa pamoja na hapo kila mtu alikuwa anamshangaa na kumpiga picha, hususani waandishi wa habari, basi na mimi ikanibidi nisogee karibu kuangalia, jamani kumbe huyu mama ni albino lakini mbona amejifungua watoto wote wana ngozi nzuri kabisa (yaani wasio albino)?

Basi nikahisi kama vile anasumbuliwa sana, na hapo nikaamua kuingilia kati na kujipa majukumu ya kuwaondoa waandishi wa habari na watu wote waliokuwa wakimshangaa katika chumba kile....haikuwa kazi rahisi sana, lakini baada ya mivutano ya kutosha, basi nikafanikiwa kuwatoa wote.

Sasa walipokuwa wameondoka, mara nikaona mtu mmoja anaingia ndani na hapo nusura nimbamize kofi maana nilidhani ni mmoja wa wale waandishi wasumbufu, basi nikashangaa tu nimekaa kimya na sisemi kitu, akafika pale akamwangalia yule mama kisha machozi yakamtoka na hapo akapiga magoti pembeni ya kitanda na kulia sana sana, na hapo kuna waandishi walitaka kulazimisha kuingia kana kwamba kulia kwa ndugu huyo nayo ni habari.
basi mimi nikabaki nimeduwaa maana simjui huyu dada au mama kwa jina wala kwa lolote na huyu naye ameingia na kuanza kulia, sasa nikajiuliza huyu kaka anahusianaje na huyu dada? na hapo nikaanza kuwaza...labda huyu kaka amewahi kujaribu kumfanyia ubaya dada huyo hivyo anajutia, au amewahi kumuokoa katika janga fulani hivyo anafurahi kwa kuona huyu dada ni mzima pamoja na matishio mengi sana ya kuuwawa kwa albino.

Sasa hapo nikawa natamani sana amalize kulia haraka ili nimsemeshe kidogo lakini haikushindikana, na hata huyu maana alikuwa kimya muda wote akinishangaa tu maskini, basi wakati nataka nikae tu,simu yangu ikaita na kupokea alikuwa ni yule rafiki yangu aliyekuwa kushonwa  na akadai amemaliza kwa hiyo anataka tuondoke zetu.......sasa hapo nilitamani nijue chochote kitu lakini haikuwezekana, basi nikatoa kadi ya mawasiliano (business card) ili nimpe yule mama, lakini akagoma kabisa kuipokea, na mimi niliwapenda sana watoto na ile adventure ya albino kuwa na watoto wanne kwa pamoja, sikuelewa kama amenifurahia au nimemboa, aana nilishindwa kutafasiri sura na ule mwangalio wake kwangu, nilitamani sana kujua stori ya maisha yake na zaidi kujua anajisikiaje, na kwakuwa alikuwa hasemi kitu, nikatamani kujua je mtu huyu ni bubu au anaongea? au ana aina fulani ya udhaifu na akilini pia, lakini wakati naendelea kujibaraguza angalau nijue mawili matatu, simu ikawa kero maana huyu rafiki yangu naye anataka kuondoka haraka, na hawezi kuniacha kwasababu funguo ninayo mimi, basi nikaamua kuondoka zangu huku moyoni nikidhamiria kuwa lazima nilete zawadi kwa watoto na mama huyo maana mimi binafsi napenda sana mapacha, Na niliamini ipo saa tutakutana tena kwa karibu na mimi nitasema nae kwa kina kuhusu maisha yake, yamkini nikapata jambo la kujifunza maana pia mimi ni mtu ninayeamini kwenye uhalisia wa maisha na sio hayo maigizo,basi nikaaga zangu (Japo sikupata muitikio wowote, japo wa macho tu) na wakati ndio natoka tu nilipofika mlangoni, wakati nafungua tu mlangoni NILISHTUKA SANA, nusura nianguke kwa mshtuko na mshangao maana punde tu bila kutarajia kabisa nikagongana uso kwa uso na ...................ITAENDELEA!!

(Je unajua niligongana uso kwa uso na nini? Unaweza ukajitahidi kuhisia kodogo?,Unafikiri yule kijana ni nani na alikuwa analia nini? basi tuonane hapa weekendi ili nikujuze hasa nini kiliendelea baada ya hapo.....TOA MAONI YAKO PIA.....Usijaribu kukosa!!!)

HABARI HII INAKUJIA KWA UDHAMINI MKUBWA WA Chavala Ideas Platform <http://chavalamedia.blogspot.com>
(c)2013

Na
King Chavala MC
+255 713 883 797
lacs.project@gmail.com
Facebook; King Chavala MC
Twitter @kingchavala
http://kingchavala.blogspot.com

No comments:

Post a Comment