Sunday, July 28, 2013

LAWRANCE NA WEMA MWANTIMWA, IWE HAMSA KWA VIJANA WASIOA KUOA!!!!

 UPENDO WA KWELI UNATOKANA NA MUNGU, HII NI KWASABABU MUNGU MWENYEWE NI PENDO..HESHIMA YA KIPEKEE YA MAHUSIANO YOYOTE YALE NI KUHALALISHA NA KUWA RASMI MBELE YA MUNGU NA BINADAMU....SIO KAZI RAHISI KIBINADAMU NA WALA SIO YA KUKURUPUKA HATA KIDOGO, LAKINI KAMA UKIMWAMINI MUNGU LAZIMA UTATIMIZA YOTE UNAYOTAKA KUYATIMIZA.....VIJANA WENGI SANA KWA SASA WAKO KATIKA MICHAKATO YA KUOA NA KUOLEWA NA WENGINE WAMESHAMALIZA  NA SASA WANA MAISHA YAO

LEO KIPEKEE TUNAKULETEA PICHA CHACHE TU ZA KUMBUKUMBU YA HARUSI YA MR & MRS LAWRANCE AND WEMA MWANTIMWA ILIYOFUNGWA TAREHE 14TH APRIL 2013 PALE CITY HARVEST NA HATIMAYE TAFRIJA KUFANYIKA KATIKA BUSTANI YA MAKUMBUSHO YA JIJINI DAR ES SALAAM...HARUSI HIYO ILIYOKUWA YA KIPEKEE SANA CHINI YA MWENYEKITI NOEL TENGA NA KAMATI YAKE NA MAANDALIZI NA KUENDESHWA NA MA-MC SAMUEL SASALI PAMOJA NTOKE BABU, BASI HIZI NI PICHA CHACHE TU ZA HARUSI HIYO!!

NA WEWE ZIKUTIE HAMASA ILI UJIFUNZE NINI MAANA YA UPENDO WA KWELI NA HESHIMA YA KUOA ....KARIBU SANA!!!
 SIKU LAWRANCE ALIPOMVIKA WEMA PETE  YA UCHUMBA KATIKA KANISA LA CITY HARVEST,JIJINI DAR ES SALAAM!
MAHARUSI,WASIMAMIZI NA WAPAMBE WOTE
ULICHEZWA SANA UKUTI UKUTI WA KICHAGA

 NA HII PICHA YA PAMOJA YA WAPAMBE WA KIKE
SAFARI YA MAISHA NDIO IMEANZA NA FUTURE NDIO ILEEEEE....

Safi saaaana


Lawrance akimlisha mkewe.

Wema akimlisha Mumewe


MR & MRS LAWRANCE AND WEMA MWANTIMWA
KWA NIABA YA UONGOZI NA WAFANYAKAZI WOTE WA BLOG HII (QUALITY-LOVE BASE), NINAWATAKIENI MAISHA MEMA, MAZURI YENYE BARAKA TELE ZA NDOA, SAWASAWA NA MLIVYOPENDANA  NA KUAPIANA KANISANI MBELE YA MUNGU NA WANADAMU, BASI UPENDO KATI YENU UZIDI KUIMARIKA KILA SIKU,AMEN!

Hotline; +255 713 883 797

Wednesday, July 24, 2013

USIKU ULE WA KWANZA WA FUNGATE (HONEYMOON)-Part 2

kwa wale wenye kumbukumbu nzuri,nilianza kuwaletea habari moja toka huko kibaha na nilikuwa kimya kwa muda ili kupata habari kamili za yote yaliyojiri, naam kwa wale ambao hawakusoma iliyopita,ninawasahuri waanzie kwanza hapa kisha tuendelee

http://quality-love.blogspot.com/2013/06/usiku-ule-wa-kwanza-wa-fungatehoneymoon.html

.......Lakini baada ya miezi mitatu nilienda tena huko kibaha ili nijue nini kinaendelea katika sakata hilo na hapo ndio nikagundua kuwa kumbe yule kijana alikuwa..........ENDELEA Part 2

*********************************************************************************

...Mtumishi aliyetumika kanisani kwa kipindi kirefu pamoja na baba yake mzazi na binti huyu,na kijana huyu kwa jinsi alivyokuwa akijitoa na kwa namna alivyohudumu na mchungaji huyo kwa muda mrefu,alipendwa sana aitha kwa utani au kwa kumaanisha mchungaji amewahi kusema..."Nitakupa zawadi ya mke toka nyumbani kwangu" na kipindi hicho mama mzazi alisikia na aliamini hivyo, sema bahati mbaya sana Mchungaji alifariki kabla ya kushuhudia binti yake anaolewa na nani.

Kwa hakika kijana alilewa katika maadili ambayo hata mabadiliko ya sayansi na tekinolojia alikemea na kuona ni dhambi....kijana huyo hakupenda TV wala hakusoma magazeti,kwake Biblia na maombi vilitosha kabisa kujua ulimwengu unaendaje.
Bado haifahamiki kuwa kijana huyu amewahi au hajawahi kuwa na mahusiano au kufanya mapenzi hapo kabla ingawa amewahi kutengwa kwa.......(nitazungumzia hapo mbeleni).
Ila kwa taarifa za mama mzazi wa binti yule, nilizopata wakati akimfokea mwanae kwa kitendo alichokifanya ni kwamba, baada ya harusi tu wakiwa kwenye gari kwenda honeymoon Kijana huyo alianza kwa kumshikashika taratibu huku akishukuru binti huyo kuolewa na yeye,inavyoonyesha kijana huyo hakumshika kwa msukumo wa kimahaba ila kwa kupata hiyo nafasi ya kuwa nae karibu sana kwa mara ya kwanza, na kwahiyo binti joto likapanda sana na kwa kuwa alikuwa yuko na mume wake aliamini usiku ule utakuwa wa kihistoria na hii ni kwasababu ya siku ile kuwa mbaya kwake (High heat katika mzunguko wake), na kwa kuwa alikuwa hajafanya kwa muda mrefu (ikumbukwe kuwa binti huyu amewahi kukengeuka na kufanya ufuska sana kabla hajarejea kundini na hivyo uzoefu wa mtaani ulikuwa mkubwa sana) na zaidi ya yote alikuwa tayari ameanza kushikwashikwa, samahani kwa lugha ya wazi lakini nimetamani ujue ukweli wote yamkini na wewe ukakusaidia kwa namna moja ama nyingine.
Basi walipofika hapo hotelini,walishushiwa zawadi zao na wale wasimamizi wakateta nao kidogo kisha wakawaacha na kuondoka zao.

Basi walipobaki peke yao,yule binti alimrukia kijana kwa kumbato la kubembea na kisha akaanza romance,lakini kijana huyu hakuonekana kupendezwa na hilo labda kwasababu hakujua na hivyo alijitahidi kuvumilia lakini hatimaye akamshusha chini na kumwambia yaliyokuwa kichwani mwake, basi binti akakubali na kuanza kusikiliza huku joto likiwa juu vibaya mno,basi yule kijana akasema natamani tumshukuru Mungu kwanza kwa sisi kufanikiwa kufunga ndoa na tuweke mikononi mwa Mungu yoote yaliyo mbele yetu,basi wakapiga magoti kando ya kitanda (huku binti akiwa na hamu yale maombi yaishe haraka),basi kijana wa watu alianza kuomba na kushukuru,akazama na kuanza kunena sana....yule binti masikini akaona hii sio akaingia kuoga na kurudi amevaa taulu,lakini mtumishi alipomwona binti na taulo ndio akaanza kukemea mapepo masalia ya uzinzi ndani ya mke wake na kuomba sana,
Binti alipochoka kusubiri akajilaza kitandani kwa hasira na kwa sababu ya uchovu na hasira kajiusingizi kakampitia......na huku baada ya maombi ya mtumishi ya takribani masaa mawili, nae akaenda kuoga na kurudi akiwa na pajama na kumkuta mkewe amepitiwa na usingizi akiwa amelalia mgongo akiwa na Taulo tu, basi hivyohivyo Mtumishi huyo akaamua kum...........ITAENDELEA!!!

(Unaweza kuhisi mtumishi aliamua kufanya nini hivyohivyo?....usijali usikose mwendelezo wa hadithi ya kweli toka kibaha,ili ujifunze kwa faida yako!!)

@Kwa hisani kubwa ya http://quality-love.blogspot.com/ (c)2013
King Chavala-MC
+255 713 883 797

Thursday, July 18, 2013

#KATIKA KUTAFUTA MWENZA#....USITAFUTE ANAYEKUFAA, BALI JITAFUTE WEWE UNAPOFAA!!!!


Habari!
Ninaamini ninaongea na mtu mzima na timamu wa akili kabisa kichwani!
Ninakushukuru hata kwa kutenga muda wako wa kujifunza kwa kusoma hapa yamkini na huko kwingineko!!
Kila jambo chini ya jua lina KANUNI zake,na kanuni hizo zikifuatwa vema huwa tunatarajia matokeo mazuri lakini kama zikikiukwa basi madhara hayaepukiki!

Na kwa kuwa sisi tumezaliwa tukiwa hatujui kitu,imetupasa kujifunza kila kitu kwa kina illi tusivunje kanuni.

Sasa ambacho huwa kinanishangaza  ni kuwa yale mambo madogo madogo ambayo hayasumbui sana maishani huwa tunatumia juhudi kubwa sana kujifunza na kisha yanayogusa kabisa mioyo yetu tunafanya kimazoea na ndio maana wengi wanaumia,maana huwa tunajiamini na kufanya kana kwamba tunajua hali hatujui....na mbaya zaidi ni kuwa hatujui na hatujui kuwa hatujui....na kama haitoshi mtu anaweza kuwa na Doctrate degree lakini bado hapa akachemka na yule msukuma mkokoteni akaukata kwa kufurahia maisha yake safi ya mahusiano.

ZINGATIA SHULE HII;

1. ASIYEJUA ALIKOTOKA HAWEZI KUJUA ANAKOKWENDA
(Yaani asiyejijua yeye mwenyewe vema,hawezi kujua maishani mwake anahitaji nini hasa)

2.ASIYEJUA AENDAKO HUWA HAPOTEI NJIA
(Anayetafuta kwa nguvu ya macho huwa haridhiki na hataacha kutafuta)

Elimu yetu imetufundisha mambo mengi lakini imetuharibu mitazamo....yaani kila mmoja anajiona yeye yuko sahihi ila mwingine yeyote yule hayuko sana na tumeandaliwa kujifunza juu ya vitu vingine tu zaidi ya sisi wenyewe na tena kuvichunguza sana kwa bidii mno kabla ya kuvifanyia maamuzi.

Ndio maana mara zote watu huwa hawazingatii kujifahamu vema,kujijua tabia zao kwa kina,kuyajua madhaifu yako na hata kujifunza kurekebishika taratibu maana inawezekana....tunabaki kutafuta huyu na yule na kazi yetu inakuwa ni kukosoa tu tabia za wengine na kusahau kuwa kuna mengine wao hufanya kama kujikinga tu kwa zile tabia zao.

MFANO;
Inawezekana sana lakini ni ngumu mno kwa mtu mwenye TABIA KUU kuhusiana na mtu mwenye TABIA KUU  kama yeye i.e Mtu muongeaji sana hawezi kukaa kwa salama na muongeaji mwingine,mtu anayependa kutuma ama kuamrisha hawezi kukaa na mtu kama yeye,hivyo ni vema mtu wa TABIA KUU akawa na Mtu wa TABIA SAWIA.

Lakini jambo la msingi sana ambalo linapaswa kuzingatiwa ni hili;
USIHANGAIKE KUTAFUTA NANI ANAKUFAA,BALI JITAMBUE NA UJIFAHAMU VEMA NA HAPO UTAJUA KWA HAKIKA WAPI UNAFAA...Maana yamkini kila unayemtaka ni TOO GOOD FOR YOU!!! ama wewe YOU ARE TOO GOOD for HIM/HER!
Sasa nafikiri ubadilishe hata namna ya utafutaji wako na uombaji wako,vinginevyo utaangukia pua

UHALISIA; Unajua kuna watu wamerukaruka weeeee halafu sasa anamtaka mtu BIKIRA(Wa kiume au wa Kike)....why Mungu akupe wewe na asimpe anayemstahili?
Na wengine wako rafu rafu tu,lakini wanataka kuhusiana na watu walio smart sana,hapana haiwezekani umeshindwa kujitunza wewe mwenyewe na kisha leo Mungu akupe treasure yake ili nayo uichakaze....Ni kweli Mungu anatupenda sana na anatuwazia mema mno lakini hawezi akaruhuru Mtoto mchanga aendeshe Hammer maana itamuua tu japo mtoto anatamani aendeshe kama wakubwa!!

HIVYO MARAFIKI NINAWSIHI SANA USILAZIMISHE URAFIKI WALA MAHUSIANO KWASABABU TU UNAMTAKA YULE AMA HUYU,LAKINI ACHA KUWA NA MAAMUZI HURU NDANI YA NAFSI YA KILA MMOJA NA HAPO NDIO MTADUMU,VINGINEVYO UNAWEZA KWENDA DUKANI KUNUNUA NATI KWA KUBAHATISHA TU,LAKINI LAITI UKIJUA BOLTI YAKO NI SAIZI NGAPI NI RAHISI KUTAFUTA NATI HUSIKA PAMOJA SPANA YA KUKAZIA!!!

AHSANTENI

King Chavala-MC
+255 713 883 797

Wednesday, July 17, 2013

MR HENRY AND ANNETH KWIYEYA HAVE NOW STARTED THEIR JOURNEY!!!




Just like a dream but it is true that my friend Henry & Anneth have already started a new journey together...Wishing you all the best and all the blessing of God in your Marriage life!!!