Monday, September 30, 2013
NA UPENDO WA KWELI NDIO HUU....KUWA SEHEMU YA IBAADA YA KUSIFU NA KUABUDU TAR 06/10/2013 NA JOHN LISU!!
UKO HAPA DVD LIVE RECORDING
NA JOHN LISSU,
06/10/2013,CCC-UPANGA, DAR ES SALAAM, TANZANIA.
SALAM TANZANIA!
Shalom Dar es salaam, Shalom Tanzania!
Ndugu wanahabari na watanzania wote kwa ujumla!
Naamini tuko salama na tunaendelea na shughuli zetu za kila
siku alizotupatia Mungu wa mbinguni, tumshukuru Mungu sana kwa Amani na utulivu
aliotupa na tuendelee kumuomba ili atuepushe na kila aina ya dhahama na
uharibifu wa Yule adui!
Kama tulivyosikia hivi karibuni, yale yaliyotokea nchi jirani
ya Kenya, kwa hakika tunawapa pole sana kwa mkasa huo, pole kwa wale
waliowapoteza wapendwa wao na wale waliojeruhika tunawaombea wapone haraka,
tunaamini hekima ya Mungu itakuwa juu ya serikali yao kushughulikia jambo hilo
kikamilifu.
Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai, hata sasa tunapoende
kumalizia robo ya tatu ya mwaka 2013, tumeshuhudia mambo mengi sana mwaka huu
ya kila aina, yapo yale yalionza kwa mara ya kwanza na mengine yamekuwa ni
mwendelezo tu wa yale yadumuyo au yalioyaanza hapo kale, tumeshuhudia michezo
mbalimbali na vipaji lukuki vikiinuka na kuimarika katika maeneo mbalimbali ya
nchi yetu, na kwa yote mema na mazuri tunampa Mungu Utukufu kwa hakika!
UTANGULIZI JUU YA JOHN LISU;
John Lisu
ni mmoja wa waimbaji/Waabudishaji wanaoheshimika katika Tasnia ya muziki wa
Injili kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa katika kukuza na kuendeleza
muziki wa Injili nchini Tanzania na nje ya Nchi. Nyimbo nyingi alizozitunga na
kuziimba zimekuwa zikitumika katika makanisa mbalimbali kama nyimbo za kusifu
na kuabudu; pia waimbaji wengine waliokua wakiimba naye wameweza kukua na
kufikia uwezo wa kuwa waimbaji wa kujitegemea. John Lisu pia ametia hamasa kubwa
miongoni wa wanamuziki wa Injili kuanza kufanya muziki wa live. John Lisu
ameweza kufanya tours za ndani ya Tanzania, Africa na Bara la Ulaya kwa ajili
ya huduma.
CHRISTINA SHUSHO |
John Lisu anategemea kufanya Project II ya
Live recoding inayojulikana kama "UKO HAPA" baada ya project ya
kwanza ya Jehova yu hai kufanya vizuri sana. Tamasha litafanyika ndani ya
ukumbi wa City Christian Centre (CCC) Upanga tarehe 6 Octoba 2013, kuanzia saa
8. mpaka saa 2 usiku.
PAUL CLEMENT |
Tamasha litasindikizwa na waimbaji nguli kama Christina
Shusho, Neema Gospel Choir, Paul Clement, Pastor Safari Paul, Bomby Johnson Waimbaji
wote wamethibitisha kuwepo.
BOMBY JOHNSON |
VENUE:
City
Christian Centre (CCC) mkabala na chuo kikuu cha mzumbe
Si
mbali saana kutoka Diamond Jubilee
MIRIUM LUKINDO WA MAUKI |
USAFIRI
(basi zilizobandikwa matangazo ya tamasha) utakuwepo kutoka posta mpya kwenda
ukumbini kuanzia saa saba na nusu mchana kwa bei ya kawaida.
PASTOR SAFARI PAUL |
HABARI NJEMA-MUHTSARI!!!!!
Sasa kwa mara pili nchini Tanzania, mwimbaji WA NYIMBO ZA
INJILI na mwabuduji JOHN LISSU wa jijini Dar Es Salaam, atakuwa anafanya Ibaada
kubwa ama Tamasha la kusifu la Kuabudu(LIVE PERFORMANCE), litakalorekodiwa moja
kwa moja (DVD LIVE RECORDING) lenye jina “UKO HAPA” (Yaani Mungu na Uwepo
wake).
Tamasha hilo litafanyika jumapili ya Tarehe 6, Octoba 2013 katika Ukumbi mkubwa wa kisasa wa Kanisa la City
Christian Centre (CCC)- Upanga, mkabala na Chuo Kikuu Mzumbe – tawi la Dar es
salaam, kuanzia saa nane mchana.
Tunataraji watu 5000
kuwa sehemu ya tamasha hili la kipekee,Utakuwa sehemu ya tamasha hilo kwa
tiketi ya 10,000/= (kawaida), 20,000/= (VIP) na 3000/= (Watoto);
na Kwale
watakaohitaji tisheti maalum za tukio hilo, basi zinapatikana kwa kati ya
12,000-15,000/=, wewe wasiliana tu na (0713905118)
NELLY-MKE WA JOHN LISU |
VITUO VYA
KUUZIA TIKETI;
1.
MWENGE
– Tarakea duka la Kanda
2.
KINONDONI
– DPC
3.
MLIMANICITY
– Silverspoon Restaurant
4.
KARIAKOO
– Mbogo Shop
5.
UKONGA
BANANA – KWA GIDO
6.
POSTA
- DUKA LA MSAMA
T-SHIRTS
-T-shirts maalumu kwa wanaume na wanawake
zinapatikana katika vituo vya kuuzia tiketi kwa bei ya elfu kumi, mpaka elfu 15(kutegmeana
na aina).
N.B; Kwa
tiketi ya VIP, mnunuzi atajipatia na Audio CD ya John Lissu ya “Uko Hapa”
USAFIRI UTAKUWEPO!!
Siku ya
tamasha kutakuwepo usafiri kutoka Posta Mpya mpaka CCC-Upanga,eneo la tukio,
hivyo kama wewe ni mgeni na hupafahamu mahali hapo, basi utakachotakiwa kufanya
ni kupanda magari toka ulipo mpaka posta mpya kabla ya saa nane,na hapo
utayakuta mabasi yenye mabango ya Tamasha, basi utajongea humo na hapo
utawezeshwa kufika eneo la tukio, muhimu ni kuzingatia muda!
MUHIMU SANA!!
JOHN LISU NA TIMU NZIMA WAKIWA MAZOEZINI |
Tamasha
hili ni muhimu sana kwa Tanzania, hasa ukizingatia JOHN LISSU ni mmoja wa
waimbaji wa kwanza kuimba live kila mahali anapoalikwa na ni mwimbaji wa kwanza
binafsi kufanya LIVE DVD RECORDING pale Ubungo plaza, na ile ya kwanza iliitwa
“JEHOVA YU HAI” na sasa anafanya LIVE RECORDING kwa viwango vingine bora zaidi,
maana Mungu hutupa hatua moja zaidi kila siku.
Ni muhimu kwa kila mtanzania kujivunia kipaji na tukio hili
muhimu katika historia, njoo umwabudu na kumsifu Mungu pamoja, Njoo ujifunze,
Njoo umuunge mkono mtanzania mwenzako na njoo uje ufanyike sehemu ya Historia
hii kwa Utukufu wa Jehova.
NEEMA GOSPEL CHOIR-KWAYA PEKEE ITAKAYOSHIRIKI "UKO HAPA" |
MWALIKO
MAALUM;
Kipekee Ninapenda kuwakaribisha wachungaji, mitume, manabii,
wainjilisti, waalimu na viongozi wote wa makanisa na huduma mbalimbali,
ninawakaribisha viongozi wote wa kisiasa na kijamii kutoka serikalini na vyama
vya siasa vyote, ninapenda kuwakaribisha wanaharakati na wanataaluma wote,
ninapenda kuwakaribisha waimbaji wote wa nyimbo za injili na wanasanaa wote,
ninapenda kuwakaribisa wanafamilia wote, asiwepo wa kubaki nyuma, ninapenda
sasa kukukaribisha wewe unaesoma hapa, naam nisaidie kumkaribisha na mwenzako
na yeye aje na mwenzake, kimsingi tukio hili ni letu wote bila kujali kitu
chochote, njooni tumsifu na kumwabudu Bwana na Mungu hataacha kuibariki
Tanzania!
EMMANUEL NDIYE ATAKAYEMPIGIA JOHN LISU LEADING GUITOR |
SHUKRANI;
Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Hakneel Production
(Wadhamini wakuu), na Jonn Lissu na timu nzima ya maandalizi; Kanisa la
CCC-Upanga; vyombo vya habari hususani Praise Power na WAPO Radio; Clouds TV
kupitia CHOMOZA na Clouds Radio kupitia GT; Sibuka Tv kupita Gospel Hits;
Bloggers hususani Christian Bloggers, magazeti na vyombo vingine vyote vya
habari! Shukrani hizi zimfikie kila mtu mmoja mmoja aliyetoa mchango wa mawazo,
fedha, ushauri, maombi, ubunifu, yaani mchango wowote wa hali na mali na Mungu
awabariki nyote!
MIRIUM LUKINDO WA MAUKI |
MUHTASARI MKUU;
Tukio; TAMASHA
LA KUSIFU NA KUABUDU, LITAKALOREKODIWA
(DVD LIVE RECORDING CONCERT)
Mhusika; JOHN LISSU
Jina: “UKO HAPA”
Mahali; UKUMBI WA KANISA LA CITY CHRISTIAN CENTRE
(CCC)- UPANGA
Lini; 06TH OCTOBA, 2013
Muda; KUANZIA SAA NANE
MCHANA
Kiingilio; Tsh 10,000/= (kawaida); 20,000/= (VIP) na
5000/= (Watoto)
Wasindikizaji;
CHRISTINA SHUSHO, MIRIUM LUKINDO, PASTOR SAFARI, BOMBY JOHNSON, NEEMA GOSPEL
CHOIR-AIC Chang’ombe na PAUL CLEMENT.
Mengineyo; USAFIRI UTAKUWEPO TOKA POSTA MPAKA CCC-UPANGA
na Unaweza kujipatia Tisheti pia.
Wahusika; WATU WOTE MNAKARIBISHWA!
UKIPATA
HABARI HII USIACHE KUMSHIRIKISHA NA MWENZAKO, NAAMINI HAUTAKOSA TUKIO HILI
MUHIMU LA KIHISTORIA KATIKA NCHI YA TANZANIA KWA UTUKUFU WA MUNGU!!
KWA PICHA
NA TAARIFA ZAIDI;
http://www.youtube.com/watch?feature=player_detailpage&v=blz0PKQ6QNU
MAWASILIANO:
O713 240 397 – JOHN
LISU
0713 905 118 –PROSPER
MWAKITALIMA – EVENT MANAGER
0713 883 797 - FREDY
CHAVALA - PUBLICITY
Imetolewa na;
Fredy E. Chavala <King Chavala (MC)>
Publicity Manager
+255 713 883 797
On Behalf of The Organizing Committee
Wednesday, September 18, 2013
PASTOR FRED AND NEEMA OKELLO'S WEDDING IN PICTURES!!!
PASTOR CHRIS OFFICIATING THE WEDDING OF FRED AND NEEMA....AND PASTOR MABINA ASIDE!
....VAA PETE HII
.......THIS IS THE CERTIFICATE TO SHOW THAT NOW WE ARE HUSBAND AND WIFE!
.....WITH MAIDS!
.....WITH PARENTS OF BOTH SIDES!
.....FRIENDS FROM TANZANIA IN UGANDA!
.....A VERY BEAUTIFUL CAKE!
....A VERY NICE VIEW OF FRED AND NEEMA'S RECEPTION ALONG LAKE VICTORIA
.....PARENTS OF FRED
.....CUTTING OF A CAKE!
.....A VERY SPECIAL MLISHANO OF CAKE!
......KUNYWA MUME WANGU!
MR AND MRS FRED AND NEEMA OKELLO |
Tuesday, September 10, 2013
"26TH OCTOBER 2013" IS NOT VERY FAR FOR THE SAKE OF SAMUEL SASALI'S MARRIAGE!!!!
Habari zenu!
Hope mnaendelea poa sana!
Hatimaye tunaendelea kuzihesabu siku kabla haijafika ile siku ambayo
SAMUEL SASALI a.k.a Papaa Sebene, Ze Blogger
atakuwa anauaga ukapela!
Kama bado hauna taarifa basi ndio habarika sasa!
na kama unatamani kuhuhudhuria tukio hilo kubwa la kihistoria basi pata kadi yako ya mwaliko na ya mchango ambayo mwisho wa kuchangia ni mwisho wa September 2013!
siku ya tar 26th October 2013 itafanyika ibaada ya ndoa pale Victory Christian Centre Tabernacle (VCCT) na kisha taafrija kufanyika jioni katika bustani nzuri ya pale Lamada Hotel!
KWA NIABA YA KAMATI YA MAANDALIZI,KWA NIABA YA BLOGGERS, KWA NIABA YA MA-MC NA KWA NIABA YANGU BINAFSI NINAPENDA KUKUKARIBISHA WEWE ULIYE MTU NA RAFIKI WA KARIBU NA UKWELI, KUWA SEHEMU YA HISTORIA.
KWA MASWALI NA MICHANGO ZAIDI USISITE KUWASILIANA KUPITIA;
0713 494110
AU 0713261425
Na King Chavala MC
+255 713 883797|
Hope mnaendelea poa sana!
Hatimaye tunaendelea kuzihesabu siku kabla haijafika ile siku ambayo
SAMUEL SASALI a.k.a Papaa Sebene, Ze Blogger
atakuwa anauaga ukapela!
Kama bado hauna taarifa basi ndio habarika sasa!
na kama unatamani kuhuhudhuria tukio hilo kubwa la kihistoria basi pata kadi yako ya mwaliko na ya mchango ambayo mwisho wa kuchangia ni mwisho wa September 2013!
siku ya tar 26th October 2013 itafanyika ibaada ya ndoa pale Victory Christian Centre Tabernacle (VCCT) na kisha taafrija kufanyika jioni katika bustani nzuri ya pale Lamada Hotel!
KWA NIABA YA KAMATI YA MAANDALIZI,KWA NIABA YA BLOGGERS, KWA NIABA YA MA-MC NA KWA NIABA YANGU BINAFSI NINAPENDA KUKUKARIBISHA WEWE ULIYE MTU NA RAFIKI WA KARIBU NA UKWELI, KUWA SEHEMU YA HISTORIA.
KWA MASWALI NA MICHANGO ZAIDI USISITE KUWASILIANA KUPITIA;
0713 494110
AU 0713261425
Na King Chavala MC
+255 713 883797|
Monday, September 2, 2013
TERABYTE LOVE (UPENDO BABKUBWA)......Part 1
Always Quality love is for Quality people!
UTANGULIZI; ......Ninakuletea cha kijana mmoja msomi mwenye shahada mbili alizozipata ughaibuni, mtaalamu ya falsafa, mtoto wa Mtumishi mkubwa wa Mungu mwenye heshima ya pekee katika jamii,Askofu wa Pentekosti ambaye pamoja na upinzani na maroroso yooote ya jamii yake alimpenda na kuamua kumuoa Dada mmoja fundi cherehani, mlutheri aliyedharaulika na ni mlemavu wa ngozi (Albino) na hata sasa wanaishi pamoja kwa furaha....unajua ilitokeaje tokeaje? Basi ungana nami taratibu tujifunze kupitia hadithi hii!
.............SIJAWAHI ONA UPENDO KAMA HUUUUUUU!
ENDELEA SASA.....
Katika maisha yangu ya pita pita hapa na pale nilikutana na jambo ambalo lilinishtua kibinadamu maana sio kawaida na nikatamani kupuuzia na nikaenda zangu,lakini nilipoondoka niliendelea kujiuliza hivi kwanini sikufuatilia kwa kina? basi tena siku zikaenda na jambo lenyewe likawa limepotea kichwani kama vile tamthilia inavyokwisha.
Basi nikajifariji ya kuwa ni jambo la kawaida tu na yamkini ni hisia zangu tu au ni maneno ya watu katika huo mtaa, maana watu nao wana visa hatari aisee!
Basi siku zimeenda na sasa imepita miaka mitatu, nikiwa nimemsindikiza mwenyeji wangu hospitali maana alijikata na bati wakati akitengeneza banda la mbwa wake, baada tu ya kupaki gari kwa mbali nikamuona kama ni mtu ninayemfahamu kwa mbali, lakini nikajiambia anyway yamkini nimechanganya tu habari, basi tukaingia hospitali na huyo ndugu yangu akasafishwa na kushwonwa na hatimaye kufungwa na pamba vema kabisa.....sasa wakati huyo ndugu yangu anasubiri kuingia theatre ili akashonwe maana palikuwa ni pakubwa sana, basi mimi niliamua kujipa tour ndani ya ile hospitali kubwa ya mkoa, ili nione ni kwa namna gani imejengwa na kupangiliwa, basi nikapiga mizunguko ya kutosha, niliporudi kwa rafiki yangu, nikakuta bado hajatoka, ndio hapo nikajiambia ngoja nikatishe kwenye moja ya mawodi, basi wakati napitta hivi mara nikamuona Dada, kimsingi ni mama kwasababu alikuwa amejifungua watoto wanne kwa pamoja na hapo kila mtu alikuwa anamshangaa na kumpiga picha, hususani waandishi wa habari, basi na mimi ikanibidi nisogee karibu kuangalia, jamani kumbe huyu mama ni albino lakini mbona amejifungua watoto wote wana ngozi nzuri kabisa (yaani wasio albino)?
Basi nikahisi kama vile anasumbuliwa sana, na hapo nikaamua kuingilia kati na kujipa majukumu ya kuwaondoa waandishi wa habari na watu wote waliokuwa wakimshangaa katika chumba kile....haikuwa kazi rahisi sana, lakini baada ya mivutano ya kutosha, basi nikafanikiwa kuwatoa wote.
Sasa walipokuwa wameondoka, mara nikaona mtu mmoja anaingia ndani na hapo nusura nimbamize kofi maana nilidhani ni mmoja wa wale waandishi wasumbufu, basi nikashangaa tu nimekaa kimya na sisemi kitu, akafika pale akamwangalia yule mama kisha machozi yakamtoka na hapo akapiga magoti pembeni ya kitanda na kulia sana sana, na hapo kuna waandishi walitaka kulazimisha kuingia kana kwamba kulia kwa ndugu huyo nayo ni habari.
basi mimi nikabaki nimeduwaa maana simjui huyu dada au mama kwa jina wala kwa lolote na huyu naye ameingia na kuanza kulia, sasa nikajiuliza huyu kaka anahusianaje na huyu dada? na hapo nikaanza kuwaza...labda huyu kaka amewahi kujaribu kumfanyia ubaya dada huyo hivyo anajutia, au amewahi kumuokoa katika janga fulani hivyo anafurahi kwa kuona huyu dada ni mzima pamoja na matishio mengi sana ya kuuwawa kwa albino.
Sasa hapo nikawa natamani sana amalize kulia haraka ili nimsemeshe kidogo lakini haikushindikana, na hata huyu maana alikuwa kimya muda wote akinishangaa tu maskini, basi wakati nataka nikae tu,simu yangu ikaita na kupokea alikuwa ni yule rafiki yangu aliyekuwa kushonwa na akadai amemaliza kwa hiyo anataka tuondoke zetu.......sasa hapo nilitamani nijue chochote kitu lakini haikuwezekana, basi nikatoa kadi ya mawasiliano (business card) ili nimpe yule mama, lakini akagoma kabisa kuipokea, na mimi niliwapenda sana watoto na ile adventure ya albino kuwa na watoto wanne kwa pamoja, sikuelewa kama amenifurahia au nimemboa, aana nilishindwa kutafasiri sura na ule mwangalio wake kwangu, nilitamani sana kujua stori ya maisha yake na zaidi kujua anajisikiaje, na kwakuwa alikuwa hasemi kitu, nikatamani kujua je mtu huyu ni bubu au anaongea? au ana aina fulani ya udhaifu na akilini pia, lakini wakati naendelea kujibaraguza angalau nijue mawili matatu, simu ikawa kero maana huyu rafiki yangu naye anataka kuondoka haraka, na hawezi kuniacha kwasababu funguo ninayo mimi, basi nikaamua kuondoka zangu huku moyoni nikidhamiria kuwa lazima nilete zawadi kwa watoto na mama huyo maana mimi binafsi napenda sana mapacha, Na niliamini ipo saa tutakutana tena kwa karibu na mimi nitasema nae kwa kina kuhusu maisha yake, yamkini nikapata jambo la kujifunza maana pia mimi ni mtu ninayeamini kwenye uhalisia wa maisha na sio hayo maigizo,basi nikaaga zangu (Japo sikupata muitikio wowote, japo wa macho tu) na wakati ndio natoka tu nilipofika mlangoni, wakati nafungua tu mlangoni NILISHTUKA SANA, nusura nianguke kwa mshtuko na mshangao maana punde tu bila kutarajia kabisa nikagongana uso kwa uso na ...................ITAENDELEA!!
(Je unajua niligongana uso kwa uso na nini? Unaweza ukajitahidi kuhisia kodogo?,Unafikiri yule kijana ni nani na alikuwa analia nini? basi tuonane hapa weekendi ili nikujuze hasa nini kiliendelea baada ya hapo.....TOA MAONI YAKO PIA.....Usijaribu kukosa!!!)
HABARI HII INAKUJIA KWA UDHAMINI MKUBWA WA Chavala Ideas Platform <http://chavalamedia.blogspot.com>
(c)2013
Na
King Chavala MC
+255 713 883 797
lacs.project@gmail.com
Facebook; King Chavala MC
Twitter @kingchavala
http://kingchavala.blogspot.com
Subscribe to:
Posts (Atom)