hABARI ZENU!!!!
Watu wengi inapofika katika swala la kutafuta mwenzi wa
maisha,nikiwa na maana mume au mke huwa inakuwa ngumu sana. Maana wanakuwa
hawajui wafanye nini ili waweze kupata ubavu ambao ndio Mungu amekusudia na sio
kuchukua ubavu wa wenzao. Ni jambo la maana sana unapotafuta au kujiandaa kuwa
na mwenzi wa maisha kujua mambo muhimu yatakayo kusaidia kuepusha kukutana na
mwenzi sahihi kutoka kwa Mungu.
Leo nitaelezea mambo muhimu matatu tu japo hii itakuwa
series ambapo tutaendelea kueleza zaidi na zaidi juu ya vitu muhimu
tunavyoendelea huko mbele.
Mambo hayo ni;
1.
Maombi
Maombi ni muhimu sana na yanakufanya uwe na
ushirika na Mungu,na unapoomba ni ishara ya kumwambia Mungu kwamba bila wewe
Mungu wangu siwezi. Kuna mchungaji mmoja alitufundisha ni muhimu kufanya maombi
pale ambapo huna picha yoyote kichwani,maana tatizo la watu wengi ni kwamba
wanakwenda kuomba Mungu huku ana picha ya mtu Fulani,au mwingine anamwambia
Mungu ooh Mungu nipe huyu,nataka kukumbia rafiki hiyo sio njia nzuri.
Wewe muombe Mungu akupe mwenzi,halafu kama
neno lake linavyosema kwamba tukiomba tuamini kwamba ametupatia na kwamba Mungu
si dhalimu maana yeye ni baba atatupa kitu chema,basi tuamini hivyo.Ukishaomba
na kuamini kwamba umepata hata kama katika hali halisi huoni anza kumshukuru
Mungu kwa mwenzi mzuri kutoka kwake.
Mtumishi mwingine alifundisha unaweza
kusema huyo mtu awe na haiba gani n.k,lakini ujue kwamba Mungu yuko juu ya
vyote atakaye kupa ndio sahihi kuliko akili yako inavyohitaji au kudhani.
Maombi ni eneo muhimu sana ni vizuri ukawa
na mtu ambaye mnaelewana na kiimani mko katika level moja au yeye amekuzidi
mkawa mnaliombea hilo pamoja na mambo mengine yanayowazunguka,maana neno lake
linasema palipo wawili watatu yeye yupo katikati yao,upako wa uwingi nao una
umuhimu sana.
Unapukuwa katika maombi ni vizuri pia
ukatubu maana unaweza ukawa na vitu vinavyozuia mawasiliano yako na Mungu. Tubu
kwa chochote ambacho umefanya kwa kujua au kutojua maana Mungu wetu ni
mtakatifu uende mbele zake ukiwa mweupe,Amen
2.
Je wewe ni mtu sahihi au unayefaa kuoa au
kuolewa
Kitu kingine cha kuangalia nafikiri ni
vizuri kujifanyia utafiti wewe mwenyewe,kujichunguza hivi kweli mimi kweli nina
tabia gani ya kufaa kuishi na mtu mwingine.
Hivi kweli mimi ninazo tabia za mke
au mume mwema kweli ?
Hivi mimi ni mtu ambaye watu wanaweza kumwamini na kumpa
moyo wake kweli?
Ni kwanini nataka kuolewa au kuoa? Nataka
kuolewa au kuoa kwasababu mama au baba
yangu anahitaji hivyo,au kwa vile rika langu wote wameolewa? Jamii inanionaje
kwanza?
Ukijitafiti utagundua kwa njia moja au
nyingine kuna mtu alishakupa mrudisho nyuma juu ya tabia zako mbaya,je kwa hizo
tabia kweli bila kuzibadilisha kuna mtu anaweza kuishi na wewe? Jiulize peke
yako wala usimuulize mtu,utapata majibu hayo utashangaa ambavyo unahitaji
ujishughulikie kwanza. Watu wengi wanalia katika maombi oooh Mungu baba
Jehova,naomba unipe mtu anayefaa kuwa mume au mke wangu lakini wao wanasahau
hivi mimi Mungu ananionaje,kweli maisha yangu yanampa Mungu utukufu. Unaweza
ukawa na vitabia ambavyo unaona kwamba si vibaya kumbe hivyo hivyo vyaweza
kusimama kama kizingiti cha Baraka zako.
Ukishajua tatizo liko wapi badilika,saa
nyingine kuna watu wanakuja na nia ya kuwa wenzi halafu wanaingia mitini basi ukijikagua
unaona inawezekana tabia hii ndio imemkimbiza,basi vizuri kufanyia kazi na sio
kukaa na kulia.
Kwakweli ni heri umlilie Mungu atakurehemu
kuliko huyo aliyekukimbia maana akishaamua ndio ameamua na kama sio ubavu wako
basi acha aende kwa ubavu wake,Amen
......TUTAENDELEA!!!! na somo hili,masomo haya
yameandaliwa na Blogger wa Rejoice and Rejoice link http://rejoice-and-rejoice.blogspot.com/